Friday, September 25, 2020

Kilimanjaro Stars yachezea kichapo

Must Read

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi...

NA MWANDISHI WETU, KAMPALA

KIKOSI cha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, kimeanza  vibaya michuano ya Chalenji, baada ya kuchapwa bao 1-0 na Kenya, Harambee Stars, uliochezwa jana kwenye Uwanja wa KCCA, jijini Kampala.

Huo ni mchezo wa kwanza kwa Kilimanjaro Stars ambao wapo Kundi B, pamoja na  Sudan na Zanzibar.

 Katika mchezo ulianza kwa kasi na Harambee Stars kuandika bao dakika ya nne kupitia kwa Hassan Abdallah Hamis.

Kilimanjaro Stars walizinduka dakika ya saba ambapo Miraji Athumani alimanusura afunge bao baada ya kupiga mpira wa faulo nje kidogo ya eneo hatari na mpira kupaa lango la Harambee Stars.

 Kilimanjaro Stars ilifanya shambulizi nzuri dakika ya 12,  lakini Mzamiru Yassin  alishindwa kufunga baada ya kupiga shuti kali ambalo lilikwenda pembeni kidogo ya lango la Harambee Stars.

Dakika ya 24 Harambee Stars  walishindwa kupata bao la pili, baada ya Abdallah kupiga shuti kali ndani ya eneo la 18  akiwa yeye na kipa Kilimanjaro Stars Aishi Manula,  lakini alipaa.

Miraji  alijaribu kupiga shuti dakika ya 44, lakini alishindwa kufunga baada ya kupaisha mpira.

Kipindi cha pili kilianza Harambee Stars waliendeleza mashambulizi na dakika ya 54 Rolence Duma almanusura afunge bao baada ya kupiga shuti kali nje kidogo ya 18 na mpira kugonga mwamba.

Dakika ya 78 Eliuter Mpepo wa Kilimamjaro Stars aliambaa na mpira hadi eneo hatari na kuachia mkwaju lakini mpira ulitua kwenye mikono ya mlinda mlango wa Kenya, Samuel Odiambo.

Baadaye Ditram Nchimbi wa Kilimanjaro Stars  alipiga shuti la mbali dakika ya 89, lakini mpira ulitoka nje.

Kilimanjaro Stars inatarajia kucheza na Zanzibar, Zanzibar Heroes kesho ikiwa ni mwendelezo wa michuano  ya Chalenji iliyoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu yao ni kuwa na mwendelezo...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi tatu kila mchezo, wakianzia mechi...

CHAMA GUMZO KILA KONA

NA WINFRIDA MTOI KIWANGO kilichoonyeshwa na kiungo wa Simba, Clatous Chama katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania...

United ‘kimeo’ yamtoa povu Evra

MANCHESTER, EnglandBEKI wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amekerwa na namna mambo yanayoendelea katika klabu hiyo, hasa ishu za usajili.
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -