Friday, January 15, 2021

Kilio cha mashabiki wa Yanga dhidi ya Juma Mahadhi

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA HUSSEIN OMAR

JUMAMOSI iliyopita lilipigwa pambano kali la kukata na shoka baina ya miamba miwili ya soka hapa nchini, Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa na timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1.

Katika pambano hilo matukio kadhaa ya kusikitisha na kufurahisha yalifanywa na wachezaji wa pande zote mbili.

Baada ya pambano hilo lililochezeshwa na mwamuzi Martin Saanya kumalizika, baadhi ya mashabiki wa Yanga walisikika wakielekeza shutuma zao kwa winga wa timu hiyo, Juma Mahadhi.

Mashabiki hao wanaamini Mahadhi ana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu yao kuibuka na ushindi katika mchezo huo lakini hakufanya hivyo.

Mashabiki hao wanaamini uwezo wa winga huyo wa kuwahadaa mabeki, mbio na mashuti vingeweza kabisa kuisaidia Yanga ambayo kikosi chake kilionekana kuwa bora zaidi mbele ya Simba.

Katika mchezo huo imani ya mashabiki wa Yanga kwa Mahadhi zilianza kupotea kadiri muda ulivyokuwa unakwenda huku wengine wakipiga kelele na kumshinikiza  kocha wa timu hiyo, Hans van der Pluijm kumtoa nje winga huyo kutokana na kushindwa kwenda sambamba na kasi ya mchezo.

Mashabiki hao walikuwa na imani kubwa na Mahadhi kutokana na kupangwa  kuanza siku hiyo katika mchezo huo, huku wakiwa na matumaini makubwa na uwezo alionao winga huyo, hata hivyo  kinyume na matarajio yao wanamwona kama ameshindwa kukata kiu zao.

Katika pambano hilo mashabiki hao wanadai Mahadhi hakucheza katika kiwango siku hiyo, lakini pia kadiri siku zinavyozidi kwenda kiwango cha mchezaji huyo kinazidi kushuka.

Kama ni hivyo basi, wakati wa Mahadhi  kukaa chini kujitathmini upya na kukumbuka kuwa kipaji pekee hakitoshi kumfanya kuwa mchezaji bora, bali anatakiwa kujituma zaidi na kutumia kila nafasi anayoipata kuthibitisha kuwa anastahili kucheza Yanga na kufika mbali zaidi.

Mahadhi anatakiwa kujifunza kutoka kwa mchezaji kama Geofrey Mwashiuya ambaye alikuwa na kipaji kikubwa sana wakati akitua Yanga, lakini mbali na majeraha ameshindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza.

Mwashiuya wakati anasajiliwa na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, mashabiki wengi walikuwa wakiamini timu hiyo imepata fundi anayetumia mguu wa kushoto ipasavyo lakini mwishoni winga huyo amepotea baada ya kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara ndani ya kikosi hicho.

Mashabiki hao wameendelea kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu juu ya hatima za wachezaji hao makinda ambao walionekana kuwa na vipaji vya hali ya juu lakini ghafla viwango vyao vimeanza kushuka kwa kasi.

Hii inamaanisha kuwa Mahadhi pia kama asipokuwa makini anaweza kujikuta akipotea na kipaji chake kikashindwa kumbeba kwenda mbele kama ambavyo alikuwa akitabiriwa wakati akitua Yanga.

Labda swali la msingi ambalo Mahadhi anatakiwa kujiuliza ni je, mchezaji kama Simon Msuva anawezaje kubaki juu kwa kipindi kirefu hivi licha ya changamoto zote anazokutana nazo? Maana kiuhalisia ukizungumzia kipaji Mahadhi anacho kikubwa kuliko Msuva.

Lakini linapokuja suala la kiwango, Msuva licha ya kila kukicha kutukanwa na mashabiki wa Yanga, ameendelea kupambana na kubaki juu kiasi cha kuendelea kumshawishi kocha Hans Pluijm amtumie bila kujali upinzani wa mashabiki.

Hivyo, Mahadhi anatakiwa kujifunza kutoka kwa Msuva ambaye kujituma kwake kumeendelea kumfanya aaminiwe Yanga, maana si kila mchezaji mwenye kipaji lazima afanikiwe wakati mwingine kujituma ni muhimu zaidi ya kipaji.

Mashabiki  wa Yanga walikwenda mbali zaidi na kuhoji kiko wapi kiwango alichokionyesha Mahadhi siku Simba ilipocheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga msimu uliopita na kupelekea kuwalaza na viatu mabeki wa Wekundu hao wa Msimbazi, Novatus Lufunga na Juuko Murshid?

“Huyu dogo anapotea sasa hivi kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele kwanini hajifunzi au mishahara mikubwa wanayopewa na viongozi ndio inawalevya,” alisikika shabiki mmoja akihoji.

Mashabiki hao waliendelea kupaza sauti zao na kwenda mbali zaidi huku wakitamani benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Pluijm mara kumi wangemsajili winga Shiza Kichuya kutokana na uwezo wake anaondelea kuonyesha uwanjani wa kiwango cha hali ya juu siku hadi siku.

Mwisho mashabiki hao walitoa ushauri kwa winga huyo kuachana na mambo ya kidunia kama anataka kufika mbali katika kazi yake ya mpira wa miguu na kumshauri kuelekeza nguvu zaidi katika kulinda kipaji chake badala ya kujiachia na mambo yasiyo na msingi kama ameanza kuyafanya.

“Kucheza Yanga si mwisho wa maisha anatakiwa ajitambue, sisi tunataka ushindi siku zote hakuna kingine maudhi kama haya tutashindwa kuyavumilia,” walimaliza mashabiki hao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -