Friday, October 23, 2020

KILO 100 ZA BALOTELLI ZAZUA TAFRANI ITALIA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

ROMA, Italia


 

KAMA unadhani vituko vimemuisha staa wa klabu ya Nice ya Ufaransa na timu ya taifa ya Italia, Mario Balotelli, basi sikia hii.

Imeripotiwa kuwa straika huyo alirejea kutoka mapumzikoni na kabla hajaanza mazoezi rasmi na wenzake, aliingia kwenye vipimo na kukutwa ameongezeka uzito hadi kufikia kilo 100 (15 zaidi ya kilo 85 halisi).

Mtandao wa L’Equipe ulidai kwamba, mfumania nyavu huyo alikutwa na uzito huo wa juu aliporudi katika majukumu ya kisoka msimu huu na kwa sasa amerejea katika klabu yake ya Nice.

Hali hiyo imetajwa kuwa ndio chanzo hata kiwango chake kuwa chini kama alivyoonekana katika mechi alizoitumikia Italia dhidi ya Poland na Ureno kiasi cha kuzomewa na mashabiki.

Na suala hilo la Balotelli lilimwibua kigogo wa chama cha soka cha Poland na nyota wa zamani wa Juventus, Zibi Boniek ambaye alikiri hali ya straika huyo haiwezi kuwa msaada kwa timu yoyote.

“Ujue baada ya Italia kucheza na Ureno, nilizungumza na Arrigo Sacchi (kocha wa zamani wa AC Milan kwa mafanikio makubwa), tulizungumza kwa kina na tulikubaliana kwamba Balotelli hakuwa tayari kucheza soka.

“Ninamwonea huruma lakini hana budi kujitunza. Inasikitisha kwa mwanasoka kutokuwa makini na hali yake mwenyewe. Na nimeshangazwa kuona kila mtu hakugundua hali hiyo,” alisema Boniek.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -