Wednesday, October 21, 2020

KILOMONI AKWAMA MAHAKAMANI

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA ZAITUNI KIBWANA

BARAZA la Wadhamini la Simba, limekwama kuweka zuio la kupinga mkutano wa dharura ulioitishwa na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kwa ajili ya kupitisha mapendekezo ya marekebisho ya katiba yao.

Mkutano wa Simba umepangwa kufanyika keshokutwa kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam, lakini jana Baraza la Wadhamini chini ya Mwenyekiti wake, Hamis Kilomoni, walikwenda kuweka zuio katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala.

Baraza hilo la Wadhamini lililofungua kesi mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Flora Mgaya, akipinga mkutano huo wa kupitisha mabadiliko ya katiba ili klabu hiyo iweze kujiendesha kisasa kwa mfumo wa hisa.

Baada ya kusikiliza hoja za waweka zuio hilo, Hakimu Flora alitupilia mbali kutokana na kiapo kilichowasilishwa na wadai wa kesi hiyo kuwa na upungufu.

Lakini sababu nyingine iliyofanya hakimu huyo kushindwa kukubaliana na hoja za wadai ni kwamba shauri hilo lilifika mahakamani hapo ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika kwa mkutano huo.

Kutokana na upungufu huo, mahakama hiyo imebariki mkutano uendelee kama ulivyopangwa na kamati ya utendaji ya klabu hiyo.

Kabla ya kwenda mahakamani kujaribu kuzuia mkutano huo, Kilomoni alisema wanachama wamekuwa wakilalamikia mkutano huo ambapo nakala za barua zimefika hadi kwa Rais John Magufuli, Waziri Mkuu, Waziri wa Michezo, Baraza la Michezo (BMT) pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hivyo kwa kuangalia kwa kina, wanaiomba Serikali kusimamisha mkutano huo.

Kilomoni na wenzake, Abdul Wahab Abas, Ally Sykes (marehemu), Ramesh Patel; wote wamekuwa wakipinga vikali mkutano huo mpaka kuamua kwenda mahakamani.

Juzi mjumbe wa kamati ya mabadiliko ya katiba Simba, Mulamu Ng’ambi, alitaja ibara na vipengele vitakavyofanyiwa mabadiliko katika mkutano huo.

Ng’ambi alisema ibara 49 ya katiba ya klabu hiyo itafanyiwa marekebisho katika vipengele sita ili iende na matakwa ya mabadiliko ya uendeshaji mpya wa klabu hiyo.

Alisema ibara hiyo imeongeza vipengele vipya ambavyo wanachama wajadili kwa kuvipitisha katika mkutano utakaokuwa wa pili baada ya wanachama kupendekeza mabadiliko katika mkutano uliofanyika miezi mitano iliyopita.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -