Wednesday, January 20, 2021

KINACHOMWEKA BENCHI MKUDE HIKI HAPA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA KIDAWA HASSAN (OUT)

MASHABIKI wa klabu ya Simba wameanza kupiga kelele juu ya kitendo cha kocha Joseph Omog kuendelea kumweka benchi kiungo Jonas Mkunde.

Nahodha huyo wa zamani wa timu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi, Mkude, hajacheza hata dakika moja katika msimu huu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting ambayo Simba walishinda mabao 7-0, mshambuliaji wao, Emanuel Okwi akifunga mabao manne,  Mkude alikuwa benchi, lakini mechi ya pili dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex hakuwamo hata benchi.

Ukiachana na mechi hizo za Ligi Kuu, lakini Mkude hakucheza hata mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa,  mechi ambayo amekuwa akifanya vizuri kila anapocheza, lakini aliishia kukaa benchi.

Pamoja na mechi hizo, lakini Mkude amekosa hata nafasi ya kuanza au hata kucheza kwenye mechi za kirafiki wakati wa kujiandaa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo mechi pekee ambayo alicheza ni ile ya Simba Day, akiingia kipindi cha pili katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na Simba kushinda bao 1-0.

Mbaya zaidi alivuliwa kitambaa cha unahodha baada ya kutumikia nafasi hiyo ya kuongoza wenzake kwa msimu mmoja pekee na kupewa Method Mwanjale, akisaidiwa na John Bocco na nahodha wa tatu akiwa ni Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.

Ni ngumu sana kuelewa ni kwanini Omog anamweka benchi mchezaji mwenye uwezo kama Mkude, hilo ni jambo ambalo linawachanganya mashabiki wa Simba, hata wale wa timu pinzani.

Wadau mbalimbali, wakiwamo baadhi ya makocha ambao walipita kwenye klabu hiyo ya Simba, nao wamejadili na kuona kuna kila sababu ya Mkude kupewa nafasi ya kucheza.

Ukiangalia kiwango cha Mkude na uchezaji wake, ni ukweli usiopingika kwamba Simba inamhitaji mchezaji huyo, ambaye ana uwezo mkubwa sana kwenye nafasi hiyo ya kiungo mkabaji.

Kwasasa kwenye timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, kiungo mkabaji pekee ambaye unaweza kumlinganisha na Mkude ni nyota wa DR Congo, ni  Papy Kabamba Tshishimbi, anayekipiga Yanga.

Mkude ni aina ya mchezaji ambaye anacheza kama kiungo mkabaji mwenye uwezo wa kuchezesha timu (deep playmaker), ni aina ya wachezaji adimu sana.

Ni kiungo ambaye mara zote anatulia na mpira na mpira ukifika kwake wenyewe unajua umefika sehemu ambayo haupaswi kudunda mpaka uruhusiwe na miguu ya Mkude.

Uwezo wake wa kumiliki mpira ni mkubwa na ana aina nyingi za kumiliki mpira kulingana na mpinzani wake anavyokuja, anaweza akautuliza mpira sehemu aliyosimama au kuucheza kwa kuupiga eneo lililowazi na kubadilisha mwelekeo wa mpira huo.

Hivyo ni vitu ambavyo wachezaji wengi hawana kwenye soka la Tanzania, hasa kwa wale wanaocheza kwenye nafasi hiyo ya kiungo mkabaji.

Mkude ana uwezo wa kucheza pasi fupi na ndefu ambazo zinaweza kutengeneza mashambulizi, uwezo wake wa kuutoa mpira sehemu hatarishi na kuuweka pazuri ni wa hali ya juu.

Ana uwezo wa kuwania mipira ya juu, kunasa pasi za wapinzani, kupora mipira akitumia nguvu na akili na kunusu eneo ambalo mpira utapigwa.

Lakini ni kwanini anawekwa benchi pamoja na ubora na uwezo alionao mchezaji huyo?

Pamoja na sifa zote hizo, lakini Mkude anasumbuliwa na nidhamu yake nje ya uwanja, jambo ambalo linamsababisha kukosa nafasi hata kwenye kikosi cha timu ya Taifa Stars, ambayo inamhitaji sana.

Ukweli ni kwamba, kuwekwa kwake benchi kwenye timu ya Taifa kunatokana na nidhamu yake, lakini kiwango chake na Himid Mao ni watu wawili tofauti.

Himid ni aina ya mchezaji anayewaza kucheza faulo au kugongana na mpinzani wake na si aina ya mchezaji mwenye uwezo wa kucheza kama Mkude.

Lakini nidhamu yake nje ya uwanja ndiyo inambeba na kumfanya Mkude kuishia benchi kila anapoitwa kwenye timu ya taifa.

Mkude amekuwa akidaiwa kujihusisha na mambo ya ulevi,  kushindwa kuhudhuria mazoezi na mara nyingine inasemekana anakutwa amekunywa siku ambayo kesho yake kuna mechi na kubakia na mning’inio wa mwisho ‘hangover’. Ni ngumu sana kwa kocha kumchezesha mchezaji wa aina hiyo, hata kama ni bora kiasi gani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -