Sunday, November 29, 2020

KING KIKI: MKONGWE WA DANSI ALIYEIMBA WIMBO WA MSIMAMO WA NYERERE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA VALERY KIYUNGU


MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa dansi, Kikumbi Mpango ‘King Kiki’, ameendelea kujizolea heshima miongoni mwa wapenzi wa muziki nchini kutokana na mambo aliyoyafanya tangu anachipukia katika fani hiyo hadi sasa.

Kati ya mambo yanayolinadi jina la nguli huyo, ni umahiri wake katika kuimba, kupiga gitaa pamoja na kutunga nyimbo zenye ujumbe matata ulioigusa jamii ya Tanzania na kwingineko.

Miongoni mwa kazi zitakazoendelea kumpa heshima kiongozi huyo wa bendi ya Wazee Sugu, ni wimbo wa Msimamo wa Nyerere, akimsifu hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere, kutokana na jinsi alivyopambana na kuiwezesha Tanzania kupata Uhuru mwaka 1961 kutoka kwa Waingereza.

Wimbo huo aliutunga mwaka 1980 wakati alipokuwa na bendi ya Orchestra Safari Sound, ambayo ilikuwa ikitumia mtindo wa Masantula Ngoma ya Mpwita ambapo baadhi ya wanamuziki alioimba nao ni Kabeya Badu, Kalala Mbwembwe, Soni Chibanda na Olai Kitunga.

Akizungumza na BINGWA hivi karibuni nyumbani kwake maeneo Mtoni kwa Azizi Ali, Dar es Salaam, King Kiki, anazungumzia mambo mengi ikiwamo fani ya muziki kuliua jina lake la asili alilopewa na wazazi wake.

“Jina langu halisi naitwa Kikumbi Mwanza Mpango, ambalo nimepewa na wazazi wangu, lingine ni Boniface ambalo nilipewa kanisani baada ya kubatizwa kwani mimi ni Mkristo. Hata hivyo, hayo yote yamekufa kwa sababu ya muziki,” anasema mkongwe huyo.

Anasema jina la King ambalo linajulikana zaidi kuliko jina lake la asili, alipewa mwaka 1979 na mashabiki wa bendi yake na wa muziki kwa ujumla, wakati alipokuwa na bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS) ‘Masantula Ngoma ya Mpwita’, siku ya uzinduzi wa bendi hiyo kwenye ukumbi wa Safari Resort, Kimara, Dar es Salaam.

Anasema siku hiyo ukumbi huo ulifurika mashabiki lukuki wakimsubiri yeye aingie ukumbi, alipofika kwenye geti la kuigilia, alilakiwa na kundi la mashabiki ambapo walimvisha joho kubwa huku wakisema kuanzia sasa jina lako unaitwa King.

King Kiki anasema alipewa jina hilo kutokana na uhodari wake katika muziki, hususani katika upangiliaji sauti za waimbaji na muziki kwa ujumla.

King Kiki akiwa ni mtoto wa tano kati ya familia ya watoto 12, alizaliwa Januari mosi, mwaka 1947 katika jimbo la Lubumbashi nchini Zaire (kwa sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC) na kwmaba alianza muziki wa rhumba mwaka 1962 nchini humo.

Anasema aliingia nchini Tanzania Juni, 1970 na kuendelea na fani yake hiyo ya muziki kwa mafanikio makubwa ambapo kwa sasa anamiliki bendi yake ya muziki wa dansi ya Wazee Sugu.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -