Wednesday, October 28, 2020

‘KING MESSI’: Mwanafunzi mwenye amri kwa mwalimu wake

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

CATALUNYA, Hispania

KWA kile kiwango alichokionesha Lionel Messi kwenye ushindi wa mabao 4-0 walioupata Barcelona dhidi ya Manchester City usiku wa kuamkia jana, ni wazi sasa staa huyo anaanza kumfundisha kazi mwalimu wake, Pep Guardiola, tena akitumia amri nzito bila huruma.

Katika mechi mbili ambazo Guardiola amerudi kwenye dimba la Camp Nou akiwa na timu tofauti, mwanafunzi wake Messi amemwadhibu bila hata chembe ya huruma.

Ndani ya mechi mbili, Guardiola amepigwa mabao 7-0 huku Messi akifunga matano. Je, utakuwa na uwezo gani wa kusema asante kwa adhabu za namna hiyo?

Yote hayo ni utani tu, lakini kilichomfanya Muargentina huyo kupiga ‘hat-trick’ ni wapi alipoyafungia na mahali gani alipojiweka uwanjani wakati wa mechi hiyo.

Wakati wa utawala wake, Guardiola aliamua kumtumia Messi kama mshambuliaji wa kati kuliko pembeni kwani alihitaji kumwona akikaa karibu na goli la mpinzani, kwani ana uwezo wa kufunga muda wowote.

Barcelona ilifanikiwa mno kwa kile alichokifanya Guardiola kwa kumtumia Messi kwenye nafasi hiyo. Mwalimu na mwanafunzi wake walikuwa kwenye ubora wao.

Mwite namba tisa wa uongo au kwa jina lolote lile, lakini Messi atabaki kuwa risasi yenye sumu ndani ya bunduki ya Barcelona na Guardiola ndiye aliyeiweka risasi hii, akaiacha, ikamuua na kumuua kwa mara ya pili.

Nyakati zinasonga na nafasi za mchezaji hubadilika pia. Alipotua Luis Suarez, Messi aliendelea kuongoza safu ya ushambuliaji akisimama katikati lakini waliamua kubadilishana nafasi na Messi akarudi kwenye winga ya kulia.

Muda mfupi baada ya uamuzi huo, Barca ikanyakua mataji matatu ndani ya miezi mitano na hata hivyo Messi amejizolea sifa nyingi kutokana na uwezo wake wa kupiga pasi za hatari tangu mfalme wa pasi duniani, Xavi Hernandez aondoke kwenye klabu hiyo.

Hapo anapewa saluti lakini Barca imejikuta ikipata wakati mgumu katika michezo kadhaa, kwani kumekuwa hakuna uwiano mzuri kwenye safu ya ushambuliaji tangu Messi asogee nyuma.

Pasi zake zimekuwa na madhara makubwa kwenye safu za ulinzi za klabu mbalimbali, lakini uwiano wake wa mabao umezidi kushuka.

Lakini kwa kile kiwango alichokionesha usiku wa juzi, kiwango cha umri wa miaka 24, alirudi kwenye ile taswira yake ya mshambuliaji hatari wa kati duniani.

Mchecheto ndani ya 18 ya City, Fernandinho akateleza, akili ya Messi ikafanya kazi haraka mno, akapachika bao la kwanza.

City wakapoteza mpira mbele ya penalti boksi kipindi cha pili, Messi akauchukua mpira, akakokota kwa sekunde kadhaa akamfunga mlinda mlango mpya, Willy Caballero.

Bao la tatu, ‘toto tundu’ Messi akaitumia vema pasi ya mwisho ya Suarez.

Messi hakuwa na presha, alifurahia mchezo, ni kama alikuwa akicheza kwenye eneo la shule na wanafunzi, maneno ya kocha wake, Luis Enrique.

Labda Guardiola hakujua kama Barca itamweka kwenye eneo alilomfundisha yeye na kumwambia: ‘Messi, kaa hapa na ufunge utakavyo’.

Au, labda Barca haikujua kuwa ‘King Messi’ angeishtua mizimu yake ya mabao. Pole Guardiola, kitanzi ulichokifunga kimekunyonga mwenyewe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -