Saturday, November 28, 2020

KIPA ALIYEKULA ‘BAGA’ SUTTON AAMUA KUJIUZULU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

MLINDA mlango wa Sutton United, Wayne Shaw, aliyenaswa na kamera akila pai (mkate kama baga) akiwa benchi wakati Arsenal wanaongoza mabao 2-0 katika mchezo wa Kombe la FA, amemwaga machozi baada ya kuamua kuondoka kwenye timu hiyo.

Kocha wa Sutton, Paul Doswell, amesema kipa huyo, Shaw ameamua kujiuzulu muda mfupi baada ya Tume ya Kamari na Chama cha Soka cha England (FA) kutangaza kumchunguza baada ya kudaiwa kwamba kampuni moja ya ‘kubet’ kuweka dau kwamba kuna mchezaji wa Sutton atakula ‘baga’ akionekana na televisheni.

Akizungumzia tukio hilo, Doswell, alisema: “Suala hilo liko mikononi mwa bodi ya timu.”

“Mwenyekiti amezungumza naye ameamua kujiuzulu. Mimi na mwenyekiti tunajisikia unyonge sana. Nimezungumza na Wayne, anamwaga machozi sana, analia sana kwenye simu. Ni jambo la huzuni sana.”

Shaw mwenye umri wa miaka 46 akiwa na uzito kama wa kilo 135, alionekana akila kwenye benchi la timu hiyo dakika chache kabla ya mchezo wao dhidi ya Arsenal ukimalizika.

Shaw alikiri kujua dau lililowekwa na kampuni ya kubeti ya Sun Bets inayomilikiwa na jarida la Sun ambao nembo yao iko kwenye jezi za Sutton.

“Ilikuwa ni viazi na nyama, nilifanya utani,” alisema Shaw kipa huyo ambaye alikanusha kufanya hivyo kwa makusudi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -