Friday, December 4, 2020

KIPIGO CHA PILI MFULULIZO:Sven akalia kuti kavu Simba

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

Wengine benchi la ufundi watajwa, yeye alia na akina Bocco, Morrison

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amezidi kujiweka katika wakati mgumu Msimbazi baada ya kikosi chake hana kupokea kipigo cha pili mfululizo Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/21, ilipofungwa na Ruvu Shooting bao 1-0 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Wekundu wa Msimbazi hao wamepoteza mchezo huo, ikiwa ni baada ya Alhamisi ya wiki iliyopita kuchapwa bao 1-0 na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga, Rukwa.

Kwa kipigo hicho, Simba imezidi kuachwa ‘solemba’ na watani wao wa jadi, Yanga, ambao juzi waliichapa KMC mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Simba inakamata nafasi ya nne ikiwa na pointi 13 kutokana na mechi saba, wakati Yanga ambao nao wameshuka dimbani mara saba, wapo nafasi ya pili na pointi zao 19, mbili nyuma ya Azam waliopo kileleni na alama zao 21.

Hata hivyo, Azam waliofungwa na Mtibwa Sugar bao 1-0 jana kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wamecheza mechi nane, hivyo iwapo Yanga wataichapa Biashara United Jumamosi, watakalia usukani wa ligi hiyo.

Kwa upande wao, ushindi wa jana umeiwezesha Ruvu Shooting kuchupa hadi nafasi ya sita katika msimamo wa ligi hiyo, ikifikisha pointi 12 baada ya kushuka dimbani mara nane.

Ruvu Shooting walipata bao lao dakika ya 36 kupitia kwa muuaji yule yule wa Wekundu wa Msimbazi, Full Maganga, aliyepokea pasi murua kutoka kwa Abdullahman Mussa.

Baada ya bao hilo, Simba walicharuka kutafuta bao la kusawazisha, lakini safu ya ulinzi ya Ruvu Shooting iliyoundwa na mabeki watatu, Juma Nyoso, Santos Mazengo na Zuberi Dabi, ilikuwa makini kuokoa hatari zote.

Mchezo huo ulianza kwa Simba kushambulia ambapo dakika ya tatu na sita, Ibrahim Ajib alikosa mabao baada ya kupata pasi za Rally Bwalya.

Dakika ya 17, Maganga wa Ruvu Shooting, alikosa bao baada ya kupokea pasi ya Mussa, lakini akiwa ndani ya 18, alipiga nje.

Dakika ya 18, Bwalya aliikosesha Simba bao, baada ya kupokea pasi kali kutoka kwa Mzamiru Yassin na kupiga shuti lililodakwa na kipa wa Ruvu Shooting, Abdallah Rashid.

Mzamiru naye alikosa bao dakika 20, akishindwa kuitumia vema pasi ya Ajib na kupiga mpira nje, kabla ya wakati dakika ya 22, Mussa kuikosesha bao Ruvu Shooting baada ya kupata pasi ya Shaban Msala.

Dakika ya 34, Luis Miquissone wa Simba, akiwa ndani ya 18, alipata mpira na kumlenga kipa wa Ruvu Shooting, Rashid aliyedaka kirahisi.

Ruvu Shooting ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Simba wakitaka kusawazisha bao na kuongeza mengine ya ushindi, lakini mabeki wa Ruvu Shooting, walisimama imara kuokoa hatari zote zilizoelekezwa langoni mwao.

Dakika 77, kulitokea tafrani na matokeo yake, Msala wa Ruvu Shooting, alitolewa nje ya uwanja baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kutokana na kucheza rafu mbaya ndani ya eneo la hatari na kuipa Simba penalti.

Penalti hiyo ilipigwa na nahodha wa Simba, John Bocco dakika ya 78, lakini shuti lake liligonga mwamba na mpira kurudi uwanjani.

Mashabiki wa Simba walijitokeza wachache tofauti na michezo mingine iliyopita, hali hiyo ikichangiwa na kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Tanzania Prisons, mjini Sumbawanga.

Akizungumzia mchezo huo, Sven alisema amekutana na timu nzuri, lakini safu yake ya ushambuliaji iliyoundwa na John Bocco, Ibrahim Ajib, Bernard Morrison na wengine, ilimuangusha, akielezea kuumizwa kwake mno na matokeo hayo.

Kwa upande wake, Kocha wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa, alisema waliingia na mpango wa kumaliza mchezo mapema, wakicheza soka aliloliita ‘Made In Tanzania’ kutokana na kikosi chake kuundwa na nyota Watanzania watupu.

Kikosi cha Simba: Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Joash Onyango, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Luis Miquissone, Mzamiru Yassin, Ibrahim Ajib, Said Ndemla (dk66), Larry Bwalya/John Bocco (dk 66) na Francis Kahata/Bernard Morrison (dk 45).

Ruvu Shooting: Abdallah Rashid, Santos Mazengo, Renatus Ambros, Juma Nyoso, Zuber Dabi, Mohammed Issa/Renatus Kisale (dk70), Abdullahman Mussa, Shaban Msala, Fully Maganga/Graham Naftar (dk 70), David Richard na Emmanuel Martin.

Wakati huo huo, habari zaidi kutoka ndani ya Simba, zinasema kuwa kipigo cha jana si tu kimemweka katika wakati mgumu Sven, bali pia baadhi ya wenzake wa benchi la ufundi, akiwamo kipa wa makipa, Mohammed Mwalami. 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -