Sunday, November 29, 2020

KISA CHA FAUSTINO NA FILAMU YA PHILLIPE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Na Kelvin Lyamuya
HAKUNA mchezaji mkubwa zaidi ya klabu. Hili neno nimelitafakari lakini kila jibu ninalopata ni kwamba, mchezaji akiamua lake hakuna wa kumzuia.

Nadharia ya mchezaji kutokuwa mkubwa zaidi ya klabu inakuja pale ambapo ni lazima heshima ya timu ibaki pale pale, isivurugwe kwa matakwa ya mchezaji mmoja.

Lakini je, akilazimisha kuondoka halafu akapewa adhabu kwa ‘nidhamu mbovu kwa mwajiri wake’, halafu ikamwachia baadaye, hapo ni nani atakuwa mkubwa? Subiri nikuelezee kitu kupitia kwa kijana Faustino.

Faustino mzaliwa wa La Plata, Argentina. Ndani ya klabu Estudiantes ndiko alikoanza kutandaza soka lake, akahamia Urusi lakini hakukaa sana akaenda Ureno na sasa yuko England.

Kiufupi huyu Faustino alitoka kwao kilomita 20 hadi Estudiantes kwenda kufanya mazoezi akijitoa kafara ili kukamilisha ndoto yake ya kuwa mwanasoka wa kimataifa. Hakutaka kuiacha ipotee angani, maana ndoto ni kama puto.

Sasa unafikiri Faustino angeiacha vipi hii ndoto? Ikiwa mtaa walioishi ulitawaliwa na maskini wa kutupwa? Baba yake alitegemea baiskeli tu kumfikisha mwanawe kufika kambini.

Angeiacha vipi ndoto hiyo ipotee ikiwa baba yake alihakikisha mwanawe anapata kila kitu anachokihitaji kwa kuuza vitu kadha wa kadha, mitaani na baada ya hapo angeanza naye safari kuelekea mazoezini huku joto na vumbi vikiwaandama njia nzima?

Si rahisi sana kwa Faustino kuiacha ndoto yake hivi hivi ikiwa baba yake mwenyewe, alisota kutoka kisoka na kuishia kucheza timu ya kawaida tu ya El Cruce kule Argentina.

Miaka 14 ya kusota huku na kule, ilimalizika kwa Faustino kutua ndani ya klabu ambayo hakudhani kama atakuwapo hadi leo, hakudhani kuwa ipo siku angeirithi jezi namba 5 ya Rio Ferdinand pale Manchester United.

Faustino Marcos Rojo hakuwa na mawazo ya kuwa ipo siku angetimiza ndoto ya kuwa mchezaji bora duniani na kuichezea moja ya timu kubwa ulimwenguni.

Hadi anafika United, Rojo alilazimisha sana kuondoka pale Sporting Lisbon baada ya United ‘kumlainisha’ kwa maneno matamu pale Marekani, wakati huo vijana wa Louis van Gaal walikuwa kwenye ziara ya mechi za kirafiki tu.

Kwanini asilazimishe kuondoka na United imekuja baada ya yeye kutoka kwenye usingizi uliotawaliwa na ndoto lukuki? Kwanini asionekane anataka kuwa mkubwa zaidi ya klabu? Sporting hawakuwa na nguvu ya kumzuia kamwe.

Mwanzoni Liverpool walikuwa na uhakika wa kumbakisha Phillipe Coutinho kwa jinsi mwenendo wao ulivyokuwa mzuri kwenye ligi, makombe mengine. Vipi sasa hivi? Mnawaelewa hawa majogoo? Pumzi imekata?

Utapataje uhakika wa kubaki na Coutinho sasa hivi? Umetolewa kwenye makombe mawili ndani ya siku saba na ubingwa wa ligi unauvizia.

Filamu itakayoanza baadaye baina ya Coutinho na Liver itautikisa ulimwengu, yule kijana wa Samba ni bidhaa adimu mno sokoni hivi sasa, huipati kirahisi.

Chelsea wana nguvu ya kumkoromea Diego Costa kwa sababu wana mwenendo safi kwenye ligi, wanayataka na makombe mengine pia, Wachina wangejitutumua kwa nguvu zote ila haikuwa kazi rahisi kumchomoa yule mtu pale wakati Antonio Conte ana mipango yake.

Waamerika Kusini wamepitia magumu mengi kuliko hawa wa UIaya. Utamlaumu vipi Rojo kwa kulazimisha kuondoka Lisbon? Utamlaumu vipi Coutinho akienda Barca?

Ndoto ya Rojo ilitimia kwa furaha na njia ya Coutinho kwenda Maracana imeanza kuupata mwanga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -