Thursday, October 29, 2020

KISA KONA YA CARLINHOS… VIGOGO YANGA WAKUTANA GHAFLA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAINAB IDDY

BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na mpira wa kona uliochongwa na Carlos Carlinhos, limewaibua vigogo wa Wanajangwani hao na kuitisha kikao kizito jana.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro, Yanga walitoka dimbani na ushindi wa bao 1-0.

Ushindi huo wa pili wa ugenini msimu huu, umeonekana kuwakuna mno wapenzi wa Yanga, hasa wakikumbuka watani wao wa jadi, Simba, waliambulia sare ya bao 1-1 kwenye uwanja huo walipowavaa Mtibwa Sugar.

Mara baada ya mchezo huo, vigogo wa Yanga, kuanzia viongozi wa klabu hiyo na wafadhili wao, walipigiana simu fasta na kupanga kukutana jana jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakupenda jina lake kutajwa, aliliambia BINGWA jana kuwa kikao hicho cha aina yake, kilifanyika katika moja ya hoteli za kifahari jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa agenda kubwa ya kikao hicho, ilikuwa ni kukutana na makocha wao, Mserbia Zlatko Krmpotic na msaidizi wake, Juma Mwambusi ili kufahamu mwelekeo wa kikosi chao na mikakati ya benchi la ufundi.

Pia, vigogo hao walipanga kuwapa makocha hao mkakati mzito kuelekea mechi zao zijazo, zaidi ikiwa ni ile ya kukata na shoka dhidi ya watani wao wa jadi, Simba inayotarajiwa kupigwa Oktoba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

“Kutokana na mwenendo wa kikosi chetu kwa sasa, tumekuja na utaratibu ambao siku moja baada ya mechi, makocha wanakaa na kurudia video za mechi tulizocheza, kisha wanakutana na Kamati ya Ufundi ambayo ina wataalamu wanaojua mpira, lengo ni kwa pamoja kuangalia wapi tulikosea na nini tufanye kwenye mechi inayokuja.

“Leo (jana) baada ya timu kuwasili Dar es Salaam ikitokea Morogoro, wakati wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja, kocha mkuu na msaidizi wapo mahali pamoja wanaangalia mechi ilivyokuwa jana,

“Lakini pia jioni ya leo (jana) watakutana na viongozi wa Kamati ya Ufundi kwa pamoja tatakuja na azimio moja ni namna gani tunaweza kuidhibiti Coastal Union baada ya kuangalia video zao za mechi za msimu huu,” alisema mtoa habari wetu huyo wa uhakika.

Alisema kuwa kupitia mpango huo, wameanza kuona mabadiliko, hasa kitendo cha Carlinhos kuanza mechi akitokea pembeni jambo ambalo wengi hawakulitarajia, ikiwa ni ushauri wa Kamati ya Ufundi inayoundwa na watu wengi wa mpira.

“Ikumbukwe hadi sasa bado kikosi cha kwanza Yanga hakijapatikana kutokana na ingizo jipya la msimu huu, benchi la ufundi wanaendelea kuwapa nafasi wachezaji tofauti tofauti hadi pale watakapopata wanachohitaji. Bila shaka Yanga itakuwa bora baada ya michezo kama sita au saba hivi,” alisisitiza.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -