Thursday, December 3, 2020

KITABU CHA GUARDIOLA: PRESHA YA KUKOSA UBINGWA YAZIDI KUMCHANGANYA-7

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

KATIKA toleo lililopita, mwandishi wa kitabu hiki aliendelea kwa kugusia presha aliyokutana nayo Guardiola katika miezi yake ya mwisho Nou Camp, kiasi cha kuuachia ubingwa wa ligi kwa mahasimu wao wakubwa, Real Madrid. Sasa endelea…

Katika mikutano na waandishi wa habari mara baada ya michezo ya ligi, Pep alikuwa haachi kulalama, kila wakati alionekana ni mtu wa kutafuta cha kujitetea, alijidhihirisha wazi kuwa alishachoka.

Kuna kitu kimoja katika maisha ambacho lazima ukutane nacho, Pep yeye alitaka kubishana na nyakati: Baada ya kipindi cha mafanikio makubwa (mataji 13 ndani ya miaka mitatu ya awali na Barca), lazima utafika wakati utateleza tu. Ni vigumu kujizoesha maisha ya ushindi iwapo unashinda kila mara bila hata kupata changamoto mpya itakayokupa funzo.

Huu ni mzunguko muhimu mno ambao alijaribu kuukwepa kwa kujipa vipindi virefu vya kazi na nadhiri za lazima.

Pep alijitesa. Hata kuijali afya yake ilikuwa ni jambo la nadra, ni hadi pale atakapojisikia sasa hali imekuwa tete kama Machi 2012, alipopatwa na tatizo la kuchomoka kwa pingili ya uti wa mgongo wake. Ni jinsi gani alivyopenda kufanya kazi bila kupumzika, kwa kiasi fulani lazima iathiri sehemu kadhaa za mwili.

José Mourinho, akiwa Madrid, aliyaona na kusikia yote hayo. Angefanya nini zaidi ya kutabasamu?

Kama ubingwa aliuchukua na aliuchukua kwa kumvuruga sana Pep, ingawa aligoma kukubali kwamba Mourinho alikuwa moja ya changamoto kubwa kwake.

Kila alipokuwa akiulizwa kitu anachokikumbuka kutoka kwenye mechi za nyuma za ‘El Clásico’ akiwa kama kocha, Guardiola alidai kusahau, si kwenye mechi za ushindi wala walizopoteza. Alishangaza. Yaani hata mauaji ya 2-6 aliyomfanyia Mourinho pale Bernabéu ameyasahau? Kisago cha mabao 5-0 alichompa Mourinho kwenye Clásico ya kwanza kwa Mreno huyo, mechi iliyotajwa kuwa bora zaidi kati ya Clasico zote, nayo aliisahau?

Kwa hakika Pep alikabiliwa na presha kubwa, si kutoka kwa Mourinho tu, bali hata vyombo vya habari vya jijini Madrid viliiponda Barcelona kuwa wachezaji wake walisaidiwa na dawa za kusisimua misuli. Kwa taarifa hizo tu, moyo wa Pep ambao ni mwepesi kusinyaa ungeruhusu kumbukumbu kufutika tu.

Kadri msimu ulivyokaribia kumalizika, uamuzi wa maisha yake ndani ya Barca usingeweza kupindishwa tena. Alikuwa mbioni kuiacha klabu ambayo ilikubalika sana ulimwenguni kutokana na jinsi alivyoiendesha.

Alichokitaka ni kuipata njia sahihi tu ya kufungua kinywa chake. Wachezaji. Na mashabiki. Lakini angewezaje? Kama wangefanikiwa kuchukua taji la Ulaya basi asingepata shida kujitokeza na kusema wazi. Na katika maamuzi yake ya kuondoka, hakumshirikisha yeyote. Hata wazazi wake hawakuwa na taarifa za awali.

Lakini kabla ya kuibuka na kutangaza uamuzi wake wa mwisho, liliibuka jambo jingine. Ni lipi hilo? Usikose toleo lijalo.
MAONI: 0712029274

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -