Friday, October 23, 2020

KITENGE AWAVULIA KOFIA JJUUKO, WAWA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA WINFRIDA MTOI

MSHAMBULIAJI wa Stand United, Alex Kitenge, ameweka bayana sababu za timu yake kushindwa kuifunga Simba kuwa ni mfumo ulioruhusu mabeki wa wapinzani wao kumbana.

Juzi Stand United ilishindwa kufurukuta mbele ya Simba baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kiwango cha juzi cha Stand kilionekana kuwa cha tofauti kabisa na namna walivyocheza dhidi ya Yanga na kufungwa mabao 4-3, huku mabao yao matatu yakifungwa na Kitenge.

Akizungumza na BINGWA baada ya mchezo wa juzi, Kitenge alisema mfumo alioutumia kocha wao ulimgharimu kwa kuwa alisimama mbele peke yake akikabiliana na mabeki wa Simba, Jjuuko Murshid na Pascal Wawa.

Alisema mfumo waliotumia haufanani na ule wa Yanga huku akieleza kuwa tangu afunge ‘hat trick’, amekuwa akikamiwa na mabeki katika kila mchezo wanaocheza.

“Nilikuwa nimesimama peke yangu hivyo  ilikuwa vigumu kuwapita mabeki wa Simba bila kuwa na msaidizi, maana nilipokuwa nikipata mpira nilishindwa kufanya chochote kutokana na kuwekewa ulinzi wa watu wa tatu,” alisema Kitenge.

Hata hivyo, Kitenge alikiri kuwa ugumu wa kuipenya ngome ya Simba ulichangiwa kuwepo kwa mabeki wenye uzoefu waliosimama vyema, hivyo ilikuwa si rahisi kwa straika mmoja kuvuka.

Matokeo ya juzi yameiwezesha Stand kushika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu baada kukusanya pointi 11 kutokana na mechi 10 walizocheza, ambapo wameshinda tatu, sare mbili na kufungwa mara tano.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -