Wednesday, October 28, 2020

KIUNGO MPYA YANGA NI BALAA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR


YANGA imemsajili kiungo mkabaji, Justin Zulu, kutoka Zesco United ya Zambia. Kiungo huyo ‘mkata umeme’ hana mambo mengi uwanjani lakini watoto wa mjini wanasema ‘ana balaa’ kubwa maana hana utani katika kutimiza majukumu yake.

Kwenye mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea, kiungo huyo amekua akitoa pasi maridadi na ameonyesha ufundi mkubwa katika kuzima mashambulizi na kunyang’anya mipira, jambo ambalo linawafanya mashabiki wa timu hiyo kuvimba vichwa.

Hata hivyo, licha ya kutajwa kuja kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite, kazi imekuwa kubwa kwani sasa kocha wa Yanga, George Lwandamina, anaumiza kichwa vilivyo kutokana na kiwango bora na kizuri anachokionyesha Twite kwenye mazoezi ya timu hiyo.

Kutokana na uwezo wa kila mchezaji, Lwandamina anaonekana kupata wakati mgumu kupitia uamuzi kwa baadhi ya wachezaji ambao wanatakiwa kuachwa na nafasi zao kuchukuliwa na wengine wapya katika usajili wa dirisha dogo litakalofungwa Desemba 15, mwaka huu.

Wachezaji wanaomuumiza kichwa ni pamoja na Twite, aliyeonyesha kiwango cha hali ya juu katika mazoezi yake ya siku saba.

Kitendo cha Twite kumshawishi Lwandamina katika mazoezi yake, anaweza kufanya uamuzi wa kumwacha Obrey Chirwa kutokana na nafasi aliyopanga kumhamishia kwa kuwa Yanga wanaye Simon Msuva.

Lwandamina amesema wachezaji aliowakuta wana uwezo wa hali ya juu na wanaweza kufanya vizuri na kutetea ubingwa wao msimu huu.

Alisema kutokana na uwezo wa wachezaji, hahitaji kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi hicho, kwani anaamini hata asipoongeza mshambuliaji mwingine katika kikosi, waliopo wataweza kumfanyia kazi nzuri kwenye ligi kuu na michuano ya Ligi ya Mabingwa mwakani.

Yanga wanatarajia kuendelea na mazoezi leo kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi hiyo utakaoanza Desemba 17, mwaka huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -