Monday, October 26, 2020

KIUNGO NAPOLI AWAONYA JUVE KUHUSU RONALDO

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

ROMA, Italia


 

KIUNGO wa Napoli, Allan  Loureiro, ameionya Juventus kuhusu ujio wa straika wao mpya, Cristiano Ronaldo, akisema kuwa wasitarajie kuwa ndio wamepata uhakika  wa kutwaa tena  ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A.

Staa huyo raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 33, alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Juve na wakaweza kuondoka na ushindi wa mabao 3-2, dhidi ya Chievo, ikiwa ni baada ya kujiunga na vinara hao akitokea Real Madrid kwa kitita cha Euro milioni 112.

Hata hivyo, pamoja na Ronaldo kushindwa kupata bao, lakini kuonekana kwake uwanjani kulisababisha idadi kubwa ya watazamaji kuushuhudia mtanange huo na inasemekana watazamaji milioni 2.3 waliushuhudia kwa njia ya televisheni.

Kutokana na hali hiyo, Allan, ambaye alikuwamo kwenye kikosi cha Napoli  kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-1  dhidi ya Lazio, anasema kuwa anafurahia ujio wa  Ronaldo, kwa kile alichodai ataleta ushindani katika ligi hiyo, lakini anasema kwamba mchezaji mmoja hawezi kuwapa uhakika wa kutwaa ubingwa.

Ujio wake nchini Italia utatuongezea idadi ya watazamaji na ndiyo itakuwa moja ya sababu na sisi tukapambana,” alisema staa huyo wa zamani wa timu ya Udinese.

“Sawa ni muhimu kuwa na mchezaji ambaye ameshatwaa tuzo nyingi za kuwa mchezaji bora wa dunia nchini Italia. Na hii inaonesha klabu zetu zimeanza kurejea kwenye matumizi na kusaka mataji,” aliongeza staa huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -