Thursday, December 3, 2020

KIUNGO ZANACO AMNG’ATA SIKIO LWANDAMINA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA MARTIN MAZUGWA

KIUNGO wa Zanaco ya Zambia, Zimiseleni Moyo, amemng’ata sikio Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, baada ya Wanajangwani hao kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imetolewa kwenye michuano hiyo baada ya kutoka sare tasa katika mchezo wa marudiano uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Mashujaa, Lusaka na Zanaco kusonga mbele kwa faida ya mbao la ugenini.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Machi 11, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.

Hata hivyo, baada ya mchezo wa juzi, Moyo ambaye ni raia wa Zimbabwe, alimtaka Lwandamina kufanya marekebisho makubwa katika idara ya ushambuliaji.

Moyo aliiambia BINGWA kwa simu kuwa, Lwandamina anatakiwa kufanya marekebisho katika safu ushambuliaji, ambayo imekosa umakini kama wanahitaji kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa.

“Yanga ina muunganiko mzuri wa timu, lakini tatizo lipo katika umaliziaji, washambuliaji wake bado hawana umakini wanapofika karibu na lango,” alisema.

Moyo alisema Yanga inawachezaji wenye vipaji vya soka na uwezo mkubwa wanatakiwa kupambana na kuacha papara wanapofika karibu na lango, kwani ndio sababu wanashindwa kupata matokeo mazuri.

Alisema kama kocha huyo atafanyia kazi eneo hilo, Yanga itafanya vizuri katika Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -