Wednesday, October 21, 2020

KIWANGO CHAMKUNA KOCHA URUSI

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

SOCHI, Urusi

KOCHA wa timu ya Taifa ya Urusi, Stanislav Cherchesov, amesema kwamba amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na timu yake ambacho kiliwasaidia kuondoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Uturuki katika michuano ya timu za Taifa.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa juzi katika Uwanja wa Fisht ulipo mjini Sochi mbele ya mashabiki 38,288, Urusi ilipata bao lake la kwanza dakika ya 20 kipindi cha kwanza lililowekwa kimiani na nyota wao, Roman Neustadter.

Bao hilo ni la kwanza kwa staa huyo kuifungia timu ya taifa tangu alipopewa uraia wa nchi hiyo kabla ya fainali za Mataifa ya Ulaya, Euro 2016 na hiyo ilikuwa ni mechi yake ya 10 kukichezea kikosi hicho.

Bao la pili la Urusi lilipatikana dakika ya 78 kupitia kwa kiungo wao, Denis Cheryshev.

Akizungumza mara baada ya mtanange huo, Cherchesov, alisema kwamba ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na vijana wake na hivyo ana matumaini watafanya vizuri katika mchezo ujao dhidi ya Sweden ambao umepangwa kupigwa Novemba 20 mjini    Stockholm.

“Kwa ujumla nimeridhishwa na kiwango kilichooneshwa na vijana wangu, hivyo nina matumaini tutafanya vizuri zaidi katika mchezo wetu ujao dhidi ya Sweden,” alisema kocha huyo.

 

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -