Friday, October 23, 2020

Klabu zifanye usajili kulingana na matakwa ya kocha

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

HIVI sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kupisha msimu wa usajili wa dirisha dogo ambao unafanyika hivi sasa, ikiwa ni hatua za timu mbalimbali kuweza kuimarisha vikosi vyao.

Huu ni msimu muhimu kwenye ligi yetu ambao kama timu ikikosea, hapa inaweza kujikuta ikipata matatizo makubwa zaidi kutokana na ukweli kwamba, hakuna wakati mwingine wa usajili zaidi ya huu.

BINGWA tukiwa ni mdau muhimu wa soka, tunaziasa klabu zilizopo kwenye ligi hiyo kuhakikisha kuwa zinafanya usajili kulingana na mahitaji ya dawati la ufundi.

Ni kawaida kwa klabu za Tanzania kufanya maamuzi, hasa ya usajili, kwa kuzingatia matakwa ya viongozi na si matakwa ya dawati la ufundi au makocha.

Hili ni jambo ambalo klabu zinafaa kuliangalia kwa makini, zama za kuangalia viongozi wanataka nini waachane nazo, bali wasimamie kwenye weledi.

BINGWA tunaona kwamba makosa makubwa yamekuwa yakifanywa na viongozi kwa kufanya usajili ambao hauna faida kwa timu na ikitokea yameibuka matatizo, anayewajibishwa ni kocha.

Hili ni kosa ambalo kocha anawajibishwa wakati yeye hahusiki na wala hakuhusika, ila kwa sababu imekuwa ni utamaduni wetu kama nchi wapo baadhi ya makocha nao wamekuwa wakiamini hakuna tatizo na ndiyo kawaida.

Lakini ukweli wa mambo ni kwamba, klabu za Tanzania zinastahili kubadilika, zinafaa kuwa na mwelekeo wa kisasa na kuachana na mambo ya kizamani na kuendesha soka kwa mazoea.

Muda huo umekwisha na kinachotakiwa ni kusimamia na kuheshimu taaluma za watu, kwa maana kuwapa makocha heshima yao ya kufanya usajili wao wenyewe badala ya viongozi.

Huu ndio weledi ambao BINGWA tunausimamia na kuuamini, kwamba unaweza kubadili mfumo wetu wa soka la Kitanzania kutoka mfumo wa kiholela na kuwa mfumo wa kisasa kama zilivyo nchi nyingine duniani.

Mwisho ni kwamba, BINGWA tunazitakia kila la heri timu zote zinazofanya usajili wakati huu wa dirisha dogo, kwani usajili ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya timu zetu kitaifa na kimataifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -