Friday, September 25, 2020

KLINIKI YA WACHEZAJI AIRTEL ILETE TIJA

Must Read

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi...

WACHEZAJI bora walioibuka katika mashindano ya Airtel Rising Stars, leo wanatarajiwa kuanza kliniki ya wiki moja ya mafunzo maalumu kuhusiana na masuala ya soka  yatakayofanyika jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), yaliyolenga kuibua vipaji chipukizi vya soka nchini.

Nyota 65 wa mashindano hayo kutoka timu mbalimbali zinazoshiriki Airtel Rising Stars watakuwa chini ya makocha wa timu za taifa.

Tunaamini mafunzo hayo yatakuwa ni sehemu mojawapo ya vijana hao kujua zaidi masuala ya soka na sheria zake, baada ya vipaji vyao kuonekana kupitia mashindano ya Airtel Rising Stars.

Nyota hao waliopata kuonekana ni kama wameanza safari yao katika maisha ya soka na tunadhani kliniki hiyo imefika katika wakati mwafaka, kwani tunatarajia wataondoka na ufahamu mkubwa baada ya kumaliza mafunzo hayo.

Sisi BINGWA tunaamini kwa mafunzo hayo, yataleta tija kwa taifa yakizingatia vipaji vya vijana hao, vitasaidia kutengeneza timu bora ya Taifa ambayo itashiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Ni  matumaini yetu kwamba mafunzo hayo yatawasaidia vijana hawa kupata mbinu za mpira, lakini pia kuziwezesha timu zetu kupata wachezaji bora kwa ajili ya vikosi vyao.

Tunapenda kuwasihi wachezaji wote waliopata nafasi ya kushiriki mafunzo kuzingatia kile watakachofundishwa na makocha hao ili waweze kuondoka na ujuzi kichwani.

Tunasema kwamba wachezaji hao wanatakiwa kuwa makini katika kipindi chote ambacho watakuwa katika mafunzo hayo, kwani ni fursa finyu kwao na wasitumie nafasi hiyo kuichezea ili baadaye waondoke na kitu baada ya kumaliza mafunzo hayo.

Tunawapongeza Airtel Rising Stars kwa kuona umuhimu wa kuandaa mafunzo hayo, kwani yatawawezesha vijana kujua mambo mbalimbali ambayo walikuwa hawayafahamu katika soka.

Tunawatakia kila la kheri katika mafunzo hayo yanayolenga kuinua vipaji vyao vya soka, kwani tunaamini  kwamba yataleta tija kwa taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu yao ni kuwa na mwendelezo...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi tatu kila mchezo, wakianzia mechi...

CHAMA GUMZO KILA KONA

NA WINFRIDA MTOI KIWANGO kilichoonyeshwa na kiungo wa Simba, Clatous Chama katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania...

United ‘kimeo’ yamtoa povu Evra

MANCHESTER, EnglandBEKI wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amekerwa na namna mambo yanayoendelea katika klabu hiyo, hasa ishu za usajili.
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -