Saturday, October 31, 2020

KLOPP ADAI KUTORIDHISHWA KIWANGO CHA MO SALAH

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England


 

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesema kwamba, anavyodhani staa wake, Mohamed Salah, anacheza kiwango cha chini licha ya juzi kuchangia kupatikana ushindi wa mabao  2-0 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wao wa Ligi Kuu England.

Katika mchezo huo, Salah alifanyiwa madhambi na beki wa kati wa Crystal Palace, Mamadou Sakho, wakiwa ndani ya eneo la penalti dakika za mwisho kipindi cha kwanza na kumfanya James Milner, apachike mkwaju wa penalti bao ambalo lilifanya Reds kuwa mbele.

Mbali na kusababisha penalti, ndani ya  dakika 15, nyota mwingine wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka, alilimwa kadi nyekundu, baada ya kumkwatua kwa makusudi, Salah, ambaye alikuwa akitafuta kumpigia pande, Sadio Mane.

Hata hivyo, pamoja na Salah kutoa  mchango huo, lakini alishindwa kupachika bao na huku akipoteza nafasi nyingi ikiwamo ya shuti lililogonga mwamba baada ya kupokea vizuri pasi aliyotengenezewa na Naby Keita.

“Hakuna kitu cha kusema binafsi kuhusu kiwango chake, lakini Mo Salah, anatakiwa kucheza vizuri zaidi,” alisema   Klopp katika mkutano wake na waandishi wa habari.

“Si tu kwa kushiriki kusababisha mabao mawili, anachotakiwa ni kujituma zaidi na hapo mambo yatakuwa sawa,” aliongeza kocha huyo.

Alisema kwamba, kama raia huyo wa Misri angekuwa kwenye ubora wake wangecheza vizuri zaidi kama timu na pengine yangepatikana mabao mengi zaidi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -