Friday, October 30, 2020

KLOPP: KUTOADHIBIWA NI BAHATI ILIYOJE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MERSEYSIDE, Liverpool


KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amekiri kuwa na bahati baada ya kutoadhibiwa na FA kutokana na kitendo chake cha kumfokea mwamuzi msaidizi katika mtanange baina ya timu yake na Chelsea mapema wiki hii.

Klopp alionekana akimfokea kwa ukali mwamuzi msaidizi, Neil Swabrick, mara baada ya mlinda mlango wake, Simon Mignolet, kuokosa mkwaju wa penalti wa straika, Diego Costa.

Hata hivyo, Mjerumani huyo aliomba msamaha na Swarbrick kumsamehe, huku akisema kuwa alivutiwa na ‘mzuka’ wake baada ya Mignolet kupangua penalti ile iliyokuwa ya muhimu kwa vijana wa Antonio Conte.

“Nilipoitazama picha nilijua kuwa haikuwa na mtazamo mzuri, lakini haikuwa mbaya kama ilivyoonekana na labda nilikuwa na bahati tu ya kutopewa adhabu.

“Kuna njia tofauti za kuzuia hisia, ule mchezo ulikuwa wa hisia kali na si rahisi kuzuia isikutawale.

“Sisi makocha tunapata shida, Jose (Mourinho) na hata Arsene Wenger, huwa wanapata tabu mno kwenye nyakati kama hizo.

“Huwa tunapigwa faini na muda mwingine tunaachwa huru. Huwa hatupendi kufanya hivyo, lakini ni moja ya mbinu zinazotokea uwanjani.

“Nilivyokuwa bado mdogo ndio nilipata tabu mno. Sasa hivi nimepunguza,” alisema Klopp.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -