Thursday, December 3, 2020

K’njaro Queens na hadithi yetu ya kupenda ngoma tusiyoiwamba

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA HASSAN DAUDI

UKIONA mtu anapenda sana kucheza ngoma na hataki kujifunza kuwamba ujue maendeleo yake katika fani hiyo ya uchezaji ngoma ni yenye shaka kubwa.

Watanzania wengi kisoka ni kama watu wanaopenda kucheza ngoma tu, wala hawahitaji kujua inawambwa vipi na pengine hawana mpango wa kujifunza kuwamba licha ya kufahamu ukweli na umuhimu wa kuwamba ngoma.

Wengi wamejaliwa maneno mengi kuliko vitendo. Utamaduni huo unatugharimu na utaendelea kutugharimu kwa mingi ijayo katika soka letu.

Ni wazuri sana katika porojo, ila utekelezaji ndio msumari wa moto. Asilimia kubwa tuko hivyo.

Tunatamani kufika walipofika wenzetu lakini kufuata njia walizotumia ni mtihani, imani yetu ni kwamba itatokea tu kama ‘zali’ nasi tutaibuka na kuwa juu jambo ambalo si rahisi kabisa.

Kwa kweli licha ya kuwatamani wenzetu waliopiga hatua, bado tunaamini kila kitu kinawezekana hata kama hatutakuwa na mipango thabiti. Tunaishi kwa kuhisi na si kwa mujibu wa hali halisi.

Mfano; wakati wenzetu wakitumia fedha nyingi kuwekeza katika soka ikiwemo kujenga shule za michezo ‘sports academies’, kununua vifaa vya kisasa, sisi tuliamini Marcio Maximo, alitakiwa kutufikisha anga za Brazil, Hispania na Ujerumani.

Nini kilichomkuta baada ya kushindwa kufikia ndoto zetu hizo za mchana?

Alimaliza mkataba wake na nafasi yake kwenye benchi la timu yetu ya Taifa, Taifa Stars ikachukuliwa na kocha mwingine. Tuachane na hayo.

Hivi karibuni, timu yetu ya soka ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens ilitwaa taji la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa). Wanastahili pongezi kwa hilo.

Kilimanjaro Queens walichukua ubingwa huo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Jinja, Uganda.

Niseme wazi kuwa kushinda kwa Kilimanjaro Queens kumetokana na juhudi ya hali ya juu ya wachezaji wa timu hiyo.

Ikumbukwe kuwa Kenya wamefuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanawake zitakazoanza kutimua vumbi Novemba 19 nchini Cameroon.

Kwa maana nyingine, haikuwa rahisi kwa ‘madada’ zetu kuibuka kidedea tena wakiwa ugenini. Ni ukweli usiopingika kuwa walikuwa ‘serious’ katika vita ya kulitetea taifa lao.

Lakini sasa, akizungumza baada ya kurejea nchini kocha wa timu hiyo, Sebastian Nkoma, alisema kitu ambacho kinathibitisha kile nilichokisema hapo awali kuwa huwa tunategemea kuvuna tusichokipanda.

Nilipenda jinsi ambavyo Nkoma aliweka wazi udhaifu wetu akisema kuwa timu hiyo ni kama ilitelekezwa kwenye mashindano hayo.

“Ni kama tulitekelezwa, kwani tulikuwa katika mazingira magumu sana, wenzetu walipelekwa kwenye hoteli nzuri lakini tulijipa moyo na kuvumilia kila hali tukiamini kuwa tulikwenda kuliwakilisha taifa na kweli tumefanikiwa kurudi nyumbani na kombe,” alisema kocha huyo.

Hapo ndipo maswali mengi yasiyo na majibu yanapoibuka, Shirikisho la Soka hapa nchini (TFF) halikujua kama Kilimanjaro Queens inakwenda kushiriki michuano hiyo?

Pia, kama TFF hawakuwa na taarifa za mateso waliyoyapata Kilimanjaro Queens, hiyo haionyeshi ni jinsi gani Shirikisho hilo lilivyokuwa mbali na timu hiyo ya wanawake?

Kwa hali hiyo ni wazi kuwa bado TFF haina mpango wowote katika kuhakikisha soka la wanawake linapiga hatua, ni porojo tu.

Eti baada ya kuwasili kutoka Uganda, ndipo timu hiyo ilipopelekwa kwenye Hoteli ya Courtyard ambako waliandaliwa chakula cha jioni kilichohudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Hapo ndipo unapojiuliza, ni kipindi gani wachezaji walitakiwa kupewa sapoti, wakati wa mashindano au baada ya kutwaa ubingwa?

Hilo ndilo tatizo letu, tunapenda kucheza na si kuwamba ngoma ambayo ndiyo itakayotupa mlio. Katika hatua nyingine, kwa upande wa wanaojiita mashabiki wa soka, hali ilikuwa hivyo pia.

Kilimanjaro Queens walipokelewa kwa staili ambayo kwa namna moja au nyingine haikuridhisha na imewavunja moyo wachezaji.

Hawakupata mapokezi waliyostahili hasa ukizingatia umuhimu wa kile walicholifanyia taifa na mazingira waliyopitia kufanikisha hilo.

Ni mashabiki wachache tu waliojitokeza kuwalaki mabingwa hao wa soka kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati kwa wanawake.

Ingawa taarifa zimedai kuwa hilo lilitokana na mkanganyiko wa ratiba ya kuwasili kwa mashujaa hao, lakini hiyo haikuwa sababu kubwa na ya kupewa kipaumbele.

Tukubali tu kuwa hatukuona umuhimu wa kupoteza muda kwa ajili ya akina dada hao. Ndiyo, wakati Mbwana Samatta alipoingia nchini akitokea Nigeria kuchukua tuzo yake ya Mchezaji Boa wa Ndani, ilikuwa usiku mkubwa na watu walikuwa wengi.

Kutokana na umuhimu ulioonekana kwa mchezaji wetu huyo kushinda tuzo hiyo, ilikuwa ni kama mchana kutokana na wingi wa mashabiki waliofurika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.

Ukiachana na hilo, hebu tujiulize, mbona tumekuwa mstari wa mbele kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere pindi klabu zetu zinapotangaza ujio wa makocha na wachezaji wa kigeni?

Wana umuhimu gani mbele ya wafalme wetu hawa ambao wameliletea heshima kubwa taifa letu? Klabu zetu zimefikia mafanikio gani baada ya ujio wa makocha na wachezaji hao?

Tujitafakari upya na tuone aibu kwa kile kilichofanywa na Kilimanjaro Queens. Turudi nyuma na kujiuliza, mafanikio ya Kilimanjaro Queens yanawahusu nini mashabiki na TFF? Tuwapongeze lakini tusivune walichopanda.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -