Monday, October 26, 2020

KOCHA MPYA AIPASUA ‘KICHWA’ BODI YA AZAM

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA SAADA SALIM


BAADA ya kukabidhi timu kwa makocha wa kikosi cha vijana, uongozi wa Azam FC unaonekana kupasua kichwa kutafuta kocha mkuu atakayerithi mikoba ya Mhispania Zeben Hernandes.

Azam ilisitisha mkataba wa Mhispania huyo na jopo lake ikiwa ni baada ya kuongoza timu hiyo katika michezo 18, ambayo imeshinda nane, sare sita huku ikipoteza mechi nne katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kuondoka kwa kocha huyo kumempa nafasi kocha wa timu ya vijana, Iddy Nassor `Cheche`, kubeba majukumu hayo kwa muda kipindi ambacho mabosi wa Azam wakiendelea kuhaha kumtafuta atakayebeba majukumu hayo.

Taarifa za uhakika zilizolifikia BINGWA zinaeleza kuwa tayari mmoja wa mabosi wa timu hiyo, ameanza mchakato wa kutafuta kocha mwenye sifa na rekodi nzuri katika michuano ya kimataifa na ngazi ya klabu.

Imeelezwa kuwa kigogo huyo huenda akasafiri nje ya mipaka ya Tanzania kwa kazi ya kumpata kocha anayeendana na vigezo wanavyovitaka ili waweze kurejesha heshima ya timu yao.

Awali kuliibuka tetesi zilizodai kuwa Azam wapo katika mchakato wa kumpa kibarua Mkurugezi wa Ufundi wa Yanga, Hans Pluijm, lakini baadaye wakaamua kufuta mpango huo.

“Suala la Pluijm lilikuwa awali lakini baada ya kukaa kikao cha bodi ya wakurugezi waliamua kuliondoa jina hilo katika orodha ya makocha waliowahitaji, huku bosi mkubwa akieleza nia yake ya kwenda nje kumleta kocha.”

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwapo kwa mvutano mkubwa kwa wajumbe bodi ya timu hiyo kuhusu kocha anayetakiwa huku kila mmoja alimnyooshea kidole mwenzake kabla ya kuamua kufikia makubaliano.

Wakati huo huo Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saady Kawemba, ameliambia BINGWA kuwa suala la kocha lipo chini ya bodi ya ukurugezi na haijatangaza ofa yoyote ya kuhitaji kocha.

Kuhusu taarifa zinazoenea juu ya kuhusishwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwassa, Kawemba alisema: “Hatujapata taarifa kamili kutoka kwa bodi ya wakurugezi kama inamhitaji Mkwassa na iwapo wakisema anafahamu tutakuja kuliweka hadharani,” alisema Kawemba.

Mbali na Pluijm na Mkwassa, wanaotajwa kunyemelewa na Azam wengine ni pamoja na Lamine Nd’iye (Msenegal) ambaye aliipa taji TP Mazembe katika Ligi ya Mabingwa pamoja na kocha wa timu ya Taifa ya Uganda, Milutin Sredojević  ambaye ana uzoefu na soka la Afrika.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -