Monday, August 10, 2020

Kocha Mwadui FC kubabidhi ripoti

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA ASHA KIGUNDULA

KOCHA wa Mwadui FC, Khalid Adam, amesema anatarajia kukabidhi ripoti yake ikiwa ni baada msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kumalizika hivi karibuni.

Akizungumza na gazeti hili jana, Adam alisema kuwa kwa sasa anaandaa ripoti maalum ya msimu uliopita tayari kuikabidhi kwa viongozi ili waweze kuifanyia kazi.

Alisema kuwa hiyo ndiyo kazi yake iliyobaki na kwamba baada ya hapo, viongozi wake ndio watakaokuwa na jukumu la kusajili.

Alisema kati ya mambo yatakayokuwapo katika ripoti yake hiyo, ni yale yaliyojiri ndani ya kikosi chake msimu huu, wachezaji gani wanaohitajika kubaki, wale wa kuachwa na nafasi za kuongezewa nguvu.

Adam alisema wanachoshukuru kwa sasa ni kuwa timu yao imebaki Ligi Kuu Bara, hivyo wanatakiwa kujipanga kutafuta wachezaji watakaoweza kuwaondoa katika hatari ya kushuka daraja.

“Nakabidhi ripoti kwa viongozi wangu, wataangalia mawazo yangu na kuyafanyia kazi kwa kujua nini kitaweza kutusaidia kwa ajili ya msimu ujao ambao ni muhimu kwetu kupata wachezaji watakaoweza kutoa ushindani na kutuondoa wasiwasi,” alisema Adam.

Mwadui ni moja ya klabu zilizoponea chupuchupu kushuka daraja, ikifanikiwa kupata ushindi katika mchezo wao wa mwisho kwa kuifunga Kagera Sugar mabao 2-1.

Iwapo ingefungwa katika mchezo huo, timu hiyo ingekuwa moja ya zilizoshuka daraja.

Timu zilizoshuka daraja msimu huu ni Singida United, Alliance, Ndanda FC na Lipuli.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -