Friday, October 23, 2020

KOCHA OILERS ATAJA SIRI ZA KUSHIRIKI KANDA 5

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA SHARIFA MMASI

KOCHA mkuu wa klabu ya mpira wa kikapu ya Oilers, Edward Bezuidenhout, ametaja siri tatu zitakazowawezesha wachezaji wake kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kanda ya Tano mapema mwaka huu.

Akizungumza na BINGWA juzi, Bezuidenhout alisema wachezaji wa timu hiyo wanatakiwa kuzingatia mambo makuu matatu, nidhamu, ushirikiano na kujali muda wanapokuwa mazoezini na mashindanoni.

Bezuidehout alisema wameanza mazoezi kujiandaa na Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam (RBA) inayotarajia kuanza Januari 28 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini.

Alisema ushirikiano wa wachezaji katika ligi ya mkoa na mashindano mengine utawawezesha kutimiza malengo yao ya kushiriki michuano ya Kanda Tano na mengineyo.

“Tumeanza mazoezi jana (juzi) kujiandaa na RBA inayosubiriwa kwa hamu na wadau mbalimbali wa mchezo wa kikapu, miongoni mwa mikakati mikubwa tuliyonayo ni kuhakikisha tunaufanyia kazi upungufu wote  uliojitokeza katika mashindano yaliyopita.

Bingwa wa RBA atashiriki mashindano ya taifa na malengo yetu sisi Oilers ni kulifanikisha hilo ili tupate tiketi ya kushiriki Kanda Tano, lakini yote hayo yatakamilika kama wachezaji wangu watazingatia mafunzo na nidhamu za mchezo huu,” alisema.

Timu mbili za juu za Mkoa wa Dar es Salaam zitakazotinga fainali kwenye Ligi ya RBA zitashiriki michuano ya Taifa Cup inayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) na bingwa ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kanda Tano.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -