Wednesday, October 28, 2020

KOCHA RUVU: WACHEZAJI WA KIGENI HAWATUSUMBUI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA TIMA SIKILO                |                   


 

KOCHA Mkuu wa timu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani, Abdulmutick Haji, amesema hawana hofu na changamoto watakazokutana nazo kwa timu zilizosajili wachezaji wengi wa kigeni kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Klabu ya Ruvu Shooting imefanya usajili wa kuongeza wachezaji watano na wawili kati yao walikuwa wanacheza soka la kulipwa, ambao ni Tumba Sued (Zambia) na Abadalla Kilala (Afrika Kusini) na wengine ni Agathon Anthony  kutoka Lipuli FC, Mohamed Mdoe na Renatus Morris (JKT).

Akizungumza na BINGWA jana, Haji alisema kuwa, timu iliingia kambini wiki iliyopita kujiandaa na Ligi Kuu, huku akisisitiza kwamba hawana wasiwasi na timu yoyote, kwani wanajiamini na wanaweza kupambana.

Aidha, alisema timu zilizosajili wachezaji wengi wa kigeni na wenye uwezo mkubwa zitaleta changamoto kwenye ligi, lakini hiyo haiwapi hofu kwa kuwa wanajiamini katika usajili walioufanya.

Aliongeza kuwa, wachezaji wazawa pia wakipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao katika Ligi Kuu hakuna wa kuwazuia, kwa sababu wanaweza kupambana.

“Msimu wa Ligi Kuu wa 2018/19 utakuwa wa ushindani tofauti na msimu uliopita, lakini tutahakikisha tunapambana ili kulinda heshinda heshima yetu,” alisema Haji.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -