Friday, October 30, 2020

Kocha Simba anukia Ihefu

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAINAB IDDY

ALIYEKUWA kocha msaidizi wa zamani wa timu ya Simba, Mganda  Jackson Mayanga, huenda akatua katika Klabu ya Ihefu inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mayanga aliyewahi kuifundisha timu ya Kagera Sugar, Coastal Union na kikosi cha Manispaa ya Kinondoni (KMC), anatarajiwa kurithi mikoba ya Maka Mwalwisi aliyetimuliwa na uongozi wa Ihefu kutokana na  kutoridhishwa na utendaji wake.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Klabu ya Ihefu,  zilisema wamepitia wasifu wa makocha watano zikiwamo  za kigeni wawili.

 “Kuna makocha wawili wa kigeni uongozi umeridhishwa na CV zao (wasifu)  ikiwamo ya Mayanja na kazi iliyopo ni  kufanya mawasiliano naye kuona kama atakuwa tayari kuja kufundisha kikosini kwetu.

“Uchaguzi wa Mayanja umekuja kutokana na kocha huyo kulijua soka la Tanzania, baada ya kufanya kazi katika timu tofauti hivyo kama atakuja Ihefu anaweza kutusaidia,” Kilisema chanzo chetu.

BINGWA lilimtafuta Mayanja akiwa nchini kwao Uganda, kujua ukweli wa jambo hilo, alisema  hajapata taarifa ya kuhitajika na klabu hiyo, lakini atakuwa tayari  kurejea nchini kama  kutakuwa na timu itamhitaji.

 “Bado sijapata taarifa ya kuhitajika huko, lakini ikija siwezi kukataa iwapo kama tutaafikiana juu ya yale nitakayohitaji katika misingi yangu ya kazi,” alisema Mayanga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -