Tuesday, October 20, 2020

Kocha Togo anusurika kifungo

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

LOME, Togo

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Togo, Claude LeRoy, amenusurika kwenda jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la ufisadi wakati wa usajili na badala yake ameamriwa kulipa faini.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, LeRoy, ambaye aliwahi kuifundisha Timu ya Taifa ya Ufaransa kati ya mwaka 1998 hadi 2003, alinusurika kifungo hicho juzi, baada ya Mahakama Kuu ya Strasbourg kumwamuru alipe Euro 15,000.

BBC ilieleza kuwa kocha huyo alitiwa hatiani kwa kosa la kughushi nyaraka wakati wa usajili katika kipindi cha misimu minne.

Mahakama hiyo ilimhukumu kocha huyo katika usajili wa mlinda mlango wa zamani wa timu ya Taifa ya Uruguay, Jose Luiz Chivalert, nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Peguy Luindula, staa wa zamani wa timu ya Taifa ya Senegal, Henri Camara na  straika wa zamani wa Denmark, Per Perdesen.

Mbali na kocha huyo, pia mahakama hiyo ilimhukumu Rais wa zamani wa  timu ya Racing Club de Strasbourg,  Patrick Proisy, kwenda jela kwa muda wa miezi 10 na faini ya Euro  25,000 na huku wakala wa zamani wa michezo,  Nicolas Geiger, akipigwa faini ya Euro 4,000.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -