Monday, October 26, 2020

KOCHA YANGA AOMBA KAZI KWA KAGAME

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA HUSSEIN OMAR

KOCHA wa zamani wa Yanga, Tom Saintfiet, ni miongoni mwa  makocha 52 walioomba kazi ya kuinoa timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, baada ya Johnny McKinstry kutemwa mwaka jana.

Rwanda inayoongozwa na Rais Paul  Kagame, Shirikisho la soka nchini humo (ferwafa), lilitangaza ajira  baada ya kumtema kocha huyo.

Ferwafa lipo katika mchakato wa kumpata kocha mpya ambaye aliiwezesha timu kuipeleka katika fainali za Afrika (Afcon) zilizopangwa kufanyika mwaka 2019, Cameroon.

Saintfiet ana wasifu mzuri (CV) baada ya kuiwezesha Yanga kuchukua ubingwa  katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu Kombe la Kagame, iliyofanyika mwaka 2012 jijini Dar es Salaam.

Rais wa Ferwafa, Vincent Degaule Nzamwita, aliuambia mtandao wa supersport.com kuwa siku chache zijazo watamtangaza kocha atakayeiongoza Amavubi.

“Tupo kwenye mchakato wa mwisho kumtangaza kocha wa kukiongoza kikosi chetu,” alisema Nzamwita.

Saintfeit anaungana na makocha hao 51 kufukuzia ulaji huo ulioachwa na mkufunzi.

Mwishoni mwa mwaka jana, alikabidhiwa kazi ya kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Trinidad na Tobago lakini alitemana nayo baadaye.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -