Friday, September 25, 2020

KOFFI OLOMIDE AMLILIA BABA YAKE (2)

Must Read

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi...

NA NOAH YONGOLO Email:noahyongoro@gmail.com

WIKI iliyopita nilikuletea tafsiri ya wimbo Papa N’Avait Pas D’Appareil Photo utunzi wake, Koffi Olomide.

Kona ya Bolingo moja kwa moja kutoka jijini Kinshasa ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR), inakuletea mwendelezo wa mashairi ya wimbo huo kama ifuatavyo hapa chini:-

Moto oyo miso naye etondi pinzoli / Mtu huyu ambaye macho yake yamejaa machozi; Kasi azamona se na miso ya motema / Lakini anayeona na macho ya moyoni: Kasi azomona se na miso ya momoire / Lakini anaona na macho ya kumbukumbu.

Papa ye oyo aza te lisusu / Baba ndio huyo hayupo tena; Au revoir papa ya Didi / Kwaheri baba yake na Didi; Au revoir Papa Ridaso / Kwa heri baba yake na Ridaso; Au revoir papa mama Riffa / kwaheri baba yake na mama Rifa; Au revoir papa Thierry / Kwaheri baba yake na Thierry.

Au revoir papa de Sylivie / Kwaheri baba yake na Sylivie; Au revoir papa Mopao yee / Kwaheri baba yake na Mopao.

Papa Charles Agpeba / Baba Charles Agbepa; Papa na Toutpu Roba, Johny Ko na Lines Konzo / Baba yake na Toutou Roba,na Lines Konzo.

Baada ya kuimba mashairi hayo, Koffi anaongea kidogo maneno haya: Antoine makila mabe / Antoine makila mabe; Mama abotaki nga na Kisangani, papa azalaki te / Wakati mama ananizaa Kisangani, baba hakuwepo.

Akaendelea kusema kuwa waliokuwepo ni baba yake, yaani Mzee Antoine na mama yake Alphonsine ‘Mama Amy’.

Merci papa / Asante baba; Baada ya kuyasema hayo,Olomide anaendelea tena kuimba akisema:

Boboma nga miso / Mnitoboe macho yangu; Mpo nazala na besoin lisusu te ya komona / Ili nisiwe na haja ya kuona tena, Miso emonaka bato ya mokili kasi Charles te / Macho huona watu wa duniani lakini sio Charles.

Pourquoi, pourquoi yee? / Kwanini, kwanini iwe yeye ?; Boma nga miso yee / Nitoboeni macho; Mpo natika kolela na butu / Iliniache kulia usiku.

Amy tika nayo kolela yee / Amy wacha na wewe kulia; Ndako nayo ekoma mawa koleka cimetiere / Nyumba yako imekuwa na huzuni kuzidi ile ya kaburi.

Papa Barack akende na sima ya ndako / Baba Barack alienda nyuma ya nyumba; Akozonga soki mbula oyo te, mbula oyo ya sima / Hatorudi tena mwaka huu wala mwakani.

Papa est ce que otekeli maman ekilia? / Baba kwani umemuachia mama usia?; Elekia nini otekeli maman Amy? / Umemuachia usia gani mama Amy?

Maman tika kolela sinon tokolela / Mama wacha kulia, tusije wote tukaanza tukalia; Nga nakomi koyoka Didi Stone akolela / Namsikia Didi Stone akilia.

Nga nakoma koyoka Delpirlo Murinho akolela / Namsikia Delpirlo Murinho akilia; Nga nakomi koyoka Saint James Rolls akolela koko naye / Namsikia Saint James Rolls akimlilia babu yake.

Olomide anaongea tena: Papa kende bien / Baba nenda salama; Tu ne dois rien a personne / Hudaiwi na mtu yoyote yule.

Ozalaka kaka na nyongo ya Didi Olomide / Ulikuwa na deni la Didi Olomide; Papa kende bien / Baba nenda salama.

Motema ya moto etonda bolingo / Moyo wa mtu umejaa upendo; Kasi miso naye ezangi papa / Bali macho yake yamemkosa baba; Papa oyo okomisa ye moto / Baba Yule ambaye kamlea hadi kufikia utu uzima’

Boya boboma ngai miso yee / Njooni mnitoboe macho yangu; Boya boboma ngai matoyi / Njooni mnizibe masikio yangu.

Mpo naboyi koyoka mongongo ya maman Amy azolela / Sintovumilia kumsikia mama akizidi yangu Amy akilia.

Mpo naboyi koyoka mongongo ya Didi stone akolela papa Charles / Sintovumilia kumsikia Didi stone akimlilia babu yake, baba Charles.

Boya boboma ngai miso / Njooni mnitoboe macho yangu; Mpo naboyi komona loboko ya mama / Kwa kuwa sipendelei kuona mkono wa mama yangu.

Esimbi nzete mpo papa okende na loboko nayo / Mkono wa mama yangu ukishikilia mti kwa kuwa baba haupo tena, kaondoka na mkono wake.

Olomide anaongea tena: okoki kosomba mbeto ya motuya, kasi okokikosomba mpongi te / Unaweza kununua kitanda cha bei ghali, kamwe hutoweza kununua usingizi.

Ata oza na montre ya wolo,okokoka kosomba ten tango / Hata ukiwa na saa ya dhahabu, huwezi kununua muda.

Mosolo nayo ata eleki ya Donald Trump, okoka kaka kosomba liwa te / Hata mshahara wako ukiuzidi wa Donald Trump, huwezi kununua kifo.

Mon pere est merveilleux / baba yangu ni mtu wa maajabu; Mon pere c’est e’toile du jour / baba yangu ni nyota ya nuru ya mchana.

Le bouclier / Baba yangu ni ngao; Le pere de la paix / Baba wa amani; nakeli vraiment nakeli / Nakuhitaji kwakweli.

Tukutane wiki ijayo hapa hapa kama ilivyo ada.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu yao ni kuwa na mwendelezo...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi tatu kila mchezo, wakianzia mechi...

CHAMA GUMZO KILA KONA

NA WINFRIDA MTOI KIWANGO kilichoonyeshwa na kiungo wa Simba, Clatous Chama katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania...

United ‘kimeo’ yamtoa povu Evra

MANCHESTER, EnglandBEKI wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amekerwa na namna mambo yanayoendelea katika klabu hiyo, hasa ishu za usajili.
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -