Tuesday, November 24, 2020

KOMBE LA DUNIA 2018… MATAIFA GANI KUIFUATA BRAZIL URUSI?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

BRAZIL limekuwa taifa la kwanza kujihakikishia nafasi ya kwenda Urusi kushiriki fainali za kombe la dunia zitakazofanyika mwaka ujao.

Brazil wameshafuzu kukwea pipa na kwenda Urusi, huku ikiwa ndiyo timu pekee iliyochukua taji hilo mara nyingi (5).

Lakini je, vipi kuhusu mataifa vigogo Hispania, Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi, England, kwenye safari hiyo ya kuisaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia za Urusi?

Italia, Hispania hakijaeleweka

Mataifa hayo makubwa kwenye ulimwengu wa soka yanakabana koo kwenye Kundi G.  Mpaka sasa, yakiwa na pointi 13 kila moja, hakuna taifa lililojihakikishia safari ya kwenda Urusi.

Mataifa hayo yatakutana jijini Madrid Septemba 2, mwaka huu, na hapo ndipo mbivu na mbichi itakapojulikana.

Timu itakayoshinda mtanange huo ndiyo itakayokata tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia za Urusi na nyingine italazimika kuipata nafasi hiyo kwa kucheza mchezo wa mwisho wa kuwania ‘play-off’.

Ufaransa mambo si mabaya

Ufaransa haijapoteza hata mchezo mmoja wa kuwania kufuzu safari ya kwenda Urusi mwakani.

Vijana hao wa Kocha Didier Deschamps wako kileleni mwa Kundi A, wakiwa wamewaacha kwa pointi mbili Sweden, wanaoshika nafasi ya pili.

Uholanzi hawasomeki

Katika Kundi A, ambalo kinara wake ni Ufaransa, huku Sweden wakikamata nafasi ya pili, Uholanzi wanapumulia mashine, kwani wanashika nafasi ya nne nyuma ya Bulgaria, wanaokamilisha ‘top three’.

Ureno hoi, Ujerumani, England safi

Uswis wameonekana kupania safari ya kwenda Urusi, kwani wameshinda mechi zao zote tano za kufuzu.

Uswis wako kileleni mwa Kundi B, wakiwa na tofauti ya pointi tatu na Ureno, wanaoshika nafasi ya pili.

Ujerumani, ambao wako kileleni mwa Kundi C, hawana shaka na safari ya Urusi, kwani Ireland ya Kaskazini wanaowakimbiza watahitaji pointi tano kuwafikia.

England wanaongoza Kundi F wakiwa na tofauti ya pointi nne na Slovakia, wanaoshika nafasi ya pili.

Argentina ni majanga

Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Paraguay kuwavusha Brazil, wameacha vita kali kati ya mataifa mengine ya Amerika Kusini.

Wanaokamata nafasi ya pili ni Colombia na ya tatu iko kwa Uruguay.

Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Venezuela umewawezesha Chile kukamilisha nne bora kwenye Kundi hilo.

Argentina iko nje ya ‘top four’ ambayo ndiyo nafasi inayotoa uhakika wa timu za Amerika Kusini kufuzu kwenda Urusi.

Mbaya zaidi kwa Argentina ni kwamba, licha ya kuwa nje ya nafasi za kufuzu mpaka sasa, haitakuwa na huduma ya staa wake, Lionel Messi, katika michezo mitatu ijayo.

Baada ya Messi kukaa nje katika mchezo uliopita dhidi ya Bolivia, kikosi hicho kilichapwa mabao 2-0 na Bolivia.

Ikumbukwe kuwa, ni timu nne za juu kutoka Amerika Kusini ndizo zitakazofuzu moja kwa moja kwenda Urusi na itakayoangukia nafasi ya tano itacheza mchezo wa kuwania.

Nigeria wanukia Urusi, wengine tusubiri

Baada ya kuikosa michuano ya kimataifa kwa miaka kadhaa, Super Eagles wameonyesha kiu ya kwenda Urusi kwenye fainali za kombe la dunia.

Wako kileleni mwa Kundi B kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Cameroon, walioko nafasi ya pili.

Misri wanaongoza Kundi E kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya Uganda, wanaokamata nafasi ya pili.

Vita nyingine iko Kundi A, ambapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tunisia wana pointi sita kila moja.

Ivory Coast wako kileleni mwa Kundi C, wakiwa wamewaacha pointi mbili Gabon na Morocco wanaoshika nafasi ya pili na ya tatu.

Ngoma ni ngumu pia kwenye Kundi D, ambapo Burkina Faso na Afrika Kusini zimefungana pointi (4), huku Senegal walioko nafasi ya tatu wakihitaji pointi moja pekee kuwafikia.

Kutoka Afrika, timu zitakazoshika nafasi ya kwanza katika kila kundi ndizo zitakazokata tiketi ya kwenda Urusi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -