Tuesday, November 24, 2020

KOMBE LA DUNIA 2018 ‘WAHUNI’ URUSI WALIVYOJIPANGA KUTISHIA USALAMA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MOSCOW, Urusi

KIKUNDI cha wahalifu nchini Urusi kimedai  ‘kitazingua’ wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 zitakazofanyika katika ardhi hiyo.

Hilo limeibua shaka kubwa hasa kwa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (Fifa) ambalo limekua likisisitiza hali ya usalama katika michuano yake hiyo.

“Kwa wengine itakuwa ni sherehe ya soka lakini wengine wataiona ni sherehe ya vurugu,” alisema mtu mmoja aliyevaa ‘mask’ alipokuwa akihojiwa na Shirika la Habari la Uingereza la BBC.

Hata hivyo, Rais wa Fifa, Gianni Infantino, alikanusha vitisho hivyo, akisistiza kuwa anaamini michuano hiyo itakuwa salama.

Katika kuimarisha usalama wa wachezaji, makocha na mashabiki, Infantino amesema huenda wakajipanga zaidi kuhakikisha fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2026 zinaandaliwa na zaidi ya nchi moja.

Ni kama ambavyo Fifa walifanya mwaka 2002 ambapo michuano ya Kombe la Dunia iliandaliwa na Japan kwa kushirikiana na Korea ya Kusini.

Infatino aliongeza kuwa anaamini mamlaka za Urusi zitaweka nguvu ya kutosha kuhakikisha hali ya usalama wakati wa fainali hizo za majira ya kiangazi.

Rais huyo alidai anaamini waandaji wa michuano ya mwaka 2018 hawajapuuzia vurugu zilizojitokeza katika mbio za kuwania taji la Euro 2016, ambapo mashabiki wa timu ya Taifa ya England na Urusi walichapana wakati timu zao zilipokuwa zikicheza.

“(Waandaji) wamekuwa wakiwasiliana na Uefa (Shirikisho la Soka barani Ulaya) na waratibu wa Ufaransa, lengo ni kujifunza kutoka kwa Ufaransa.

“Sina shaka kuhusu matatizo ya mwaka 2018,” alisema bosi huyo na kuongeza: “Nina imani ya kutosha kwa mamlaka za Urusi.

“Wanalichukulia suala hili kwa umakini wa hali ya juu. Wamekuwa wakiwasiliana na Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa) na Uefa.

Hata hivyo, kuna taarifa kuwa kikundi hicho cha wahuni wa Urusi kipo kwenye maandalizi mazito ikiwamo kufanya mazoezi ya ‘gym’, kuhakikisha wanaharibu utulivu wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018.

Imeelezwa kikundi hicho kimelenga zaidi kupambana na mashabiki wa soka wa England.

Itakumbukwa katika fainali za Mataifa Afrika za mwaka 2016 ‘Euro 2016’, mashabiki wa Urusi na England walichapana wakati mchezo uliozikutanisha timu zao ulipokuwa ukiendelea.

Katika mchezo huo, mashabiki wa England walikuwa na mabango yaliyokuwa yamendikwa ‘Tunaichukia Urusi’.

Katika michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2018, inadaiwa kuwa tayari kuna vikundi vingine zaidi ya 150 ambavyo vimelenga kuwashambulia mashabiki wa England watakaofika Urusi.

“Wapinzani wetu ni England, ndiyo wahuni wakubwa. Tunawasubiri. Ukiwa pale (Urusi), basi jua umekwisha,” alisema mtu mwingine ambaye pia uso wake ulikuwa umefunikwa na ‘mask’.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -