Saturday, October 31, 2020

Koscienly: Giroud ajipange Sanchez anatisha ile mbaya

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

BEKI wa Arsenal, Laurent Koscielny, amesisitiza kwamba mshambuliaji wao Olivier Giroud anaweza kurejea kwenye kikosi cha kwanza, pamoja na nyota anayecheza nafasi yake kwa sasa, Alexis Sanchez, anacheza vizuri sana.

Nyota hao wawili walichelewa kurejea kutoka kwenye michuano ya Euro 2016, lakini kwa sasa Giroud anauguza majeraha ya kidole gumba yaliyomsababishia kukosa mechi nne za Gunners.

Alexis amekuwa akichezeshwa kama mshambuliaji wa kati kutokana na kukosekana kwa Giroud na ameng’ara kwenye nafasi hiyo, akifunga mabao matano na akipika matano katika mechi tisa, lakini Koscielny amesema kwamba nyota mwenzake wa Ufaransa anaweza kurejea kwenye nafasi yake.

“Tulichelewa kurejea baada ya Euro 2016, hivyo tulipaswa kujituma zaidi mazoezini ili tuwe fiti,” alisema Koscielny alipokuwa akizungumza na waandishi kuhusiana na kuwa fiti kwa Giroud.

“Kuna ushindani katika safu ya ushambuliaji na kwa sasa Alexis Sanchez anatakata mno, hivyo ni ngumu kumtoa kwenye kikosi cha kwanza.

“Namjua Olivier na amekumbana na mambo magumu sana katika soka lake. Tunajua uwezo wake na msimu bado ni mrefu.

“Atakuwa na nafasi ya kurejea kwenye kikosi na kujibu uwanjani juu ya uwezo wake.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -