Thursday, November 26, 2020

KOTEI WA SIMBA: LIGI YA BONGO KIBOKO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SAADA SALIM

KIUNGO mbakaji wa Simba Mghana, James Kotei, amesema ameshangazwa  na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wa Ndanda katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba walishinda mabao 2-0 katika mchezo huo uliochezwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, huku Kotei alishindwa kumaliza dakika 90 baada ya kuumia.

Hata hivyo, Kotei amesema ili uweze kucheza ligi ya Bongo, mchezaji anahitaji kujituma sana kutokana na ushindani mkali wa soka aliouona kutoka kwa Ndanda.

Kotei alisema mchezo huo ulikuwa wa ushindani mkali kutokana na wachezaji wa Ndanda kutoa upinzani wa hali ya juu licha ya wao kuibuka na ushindi.

Alisema kulingana na ugumu aliokutana nao kwenye mchezo huo na mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar, ana imani soka la Tanzania lina ushindani  wa hali ya juu na mchezaji anatakiwa kupambana ili aweze kuaminiwa katika kikosi cha kwanza.

“Hii ligi ya huku ni ngumu kwa kweli, ushindani niliokutana nao siku ya kwanza si wa kawaida, timu zote zilikuwa kwenye ubora wa hali ya juu, hivyo mchezaji anatakiwa kuonyesha juhudi ili kusaidia timu yake kupata ushindi,” alisema.

Katika hatua nyingine mshambuliaji wa timu hiyo, Fredrick Blagnon, hatakuwa  nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili hadi tatu baada ya kuumia nyama za paja.

Blagnon aliumia katika mchezo uliopita dhidi ya Ndanda, ambapo ataanza kuukosa mchezo wa kesho dhidi ya JKT Ruvu utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, alisema  pamoja na kumkosa mchezaji huyo, kikosi chake kipo vizuri.

Omog alisema mchezo wao wa kwanza dhidi ya JKT Ruvu walitoka sare tasa, hivyo hataki kurudia makosa yaliyojitokeza kwani atahakikisha wanapata ushindi.

Alisema ana imani ligi ina ushindani mkali na kila mchezaji amempa majukumu yake ili kuhakikisha wanapata pointi tatu.

“Kwa sasa hakuna timu tutakayoipuuza, hakuna timu ndogo zote zinahitaji kupata pointi kupitia Simba, hivyo nimetoa maelekezo na wachezaji kuwa makini kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu katika mchezo huo,” alisema Omog.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -