Thursday, October 22, 2020

KUELEKEA MIAKA 20 YA KHADIJA YUSUPH NA VIJEMBE VINAVYONOGESHA TAARABU

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA ZAITUNI KIBWANA

UKIMUONA huwezi kuamini anachokisema, lakini ukweli ni kwamba ana miaka 20 katika muziki wa taarabu, anamudu kusimama jukwaani, kucheza na kuimba kwa zaidi ya saa nane bila kuchoka huku akifanya hivyo takribani wiki nzima.

Hapa namzungumzia mwimbaji aliyetimiza miaka 20 akiwa na bendi mbalimbali nchini, naye si mwingine ni Khadija Yusufu ‘Sauti ya Chiriku’.

Khadija aliyepitia bendi mbalimbali ikiwamo East Africa Melody ‘Watoto wa mjini’, Zanzibar  Stars, Jahazi ‘Wana nakshi nakshi’ akapita Five Stars (Watoto wa Bongo), akarudi Jahazi na sasa anaunda bendi mpya ya Wakali Wao.

BINGWA limefanya mahojiano na mwanamama huyo ambaye  huwezi kutaja muziki wa taarabu bila kuliorodhesha jina lake kwenye  muziki na kuwaacha mashabiki wakiweweseka.

Lengo la mazungumzo hayo ni onyesho lake litakalofanyika Jumapili  pale kwenye Ukumbi wa Travertine pale Magomeni jijini  Dar es Salaam.

Yapo mengi aliyozungumza ukiacha onyesho hilo ambalo limepewa jina la Usiku wa Khadija, likiwa na lengo la kusherehekea siku yake ya kuzaliwa sambamba na kutimiza miaka 20 ya uimbaji.

Nilianza kuimba nikiwa na miaka 16

Wakati Jumapili hii anatimiza miaka 20 ya uimbaji, Khadija anasema kuwa alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 16.

Anasema wimbo wake wa kwanza aliimba akiwa na kundi la East African Melody uliojulikana kwa jina la Stop.

“Kipindi hicho bado binti mdogo nilitoka na Stop, wimbo ambao kiukweli ndio nilioanza nao kwenye kundi la Melody,” anasema Khadija.

Lakini leo hii licha ya kuzunguka huku na kule nimefanikiwa kuendelea kudumu kwenye uimbaji na sasa nina miaka 20 toka nianze kazi hii.

“Nimeandaa Usiku wa Khadija, ila kubwa ni kusherehekea miaka hii 20 ya uimbaji, kama utavuta picha kuna wasanii siku hizi hawafikishi hata miaka mitano, hivyo lazima nijipongeze,” anasema.

Anasema onyesho hilo chini ya Wakali Wao litasindikizwa na wasanii mbalimbali ikiwamo bendi yake ya zamani ya East African Melody na Mc Suddy mkali wa singeli.

Vijembe ndio vinavyonogesha taarabu

Akizungumzia suala nzima kwenye nyimbo za taarabu kuwa na mafumbo, mkali huyo mwenye  sura ya kuvutia, mwenye macho yanayovutia kumtizama, anasema kuwa mafumbo ndiyo yanayobeba dhana ya taarabu.

“Mimi kawaida yangu ni kuimba tu, hivyo kijembe kinakwenda kwa mtu yeyote yule kama taarabu inavyosema,” anasema.

Atavaa Pampas Jukwaani

Gwiji huyo wa taarabu ameahidi kuvaa pampas siku hiyo kama ishara ya kusherehekea miaka yake 20 ya uimbaji, huku akitumbuiza na bendi yake ya zamani ya East African Melody.

“Kutakuwa na ‘surprise’ nyingi ila waje washuhudie ninapovaa pampas pale jukwaani, si unajua miye mtoto nimezaliwa siku hiyo,” alisema.

Bifu lake na wifi yake

Kwa kipindi cha hivi karibuni, kuliibuka maneno kati ya mke wa Mzee Yusuph, Leila Rashid na wifi yake, Khadija mara baada ya mfalme Mzee Yusuph kuachana na muziki.

 

Vita hivyo vya maneno vilianza baada ya Khadija kushtumiwa kumuimba wifi yake kwa kusema talaka inamsubiri, jambo lililotafsiriwa kuwa ni kuanzisha ugomvi na wifi yake huyo.

 

Lakini mwenyewe Khadija ametoka mafichoni na kusema kuwa: “Mimi nimeimba tu, kidongo kinakwenda kwa mtu yeyote yule, sijamuimba wifi wala mtu yeyote, mbona kuna watu pia wanasema wimbo wa Nina Moyo Sio Jiwe nimeimbwa mimi, lakini mimi naona si kweli kaka angu Mzee Yusuph hawezi kutunga nyimbo ya kuniimba,” anasema.

Mkanganyiko wa Jahazi

Bendi ya Jahazi kwa siku za hivi karibuni iliingia mkanganyiko mkubwa baada ya wasanii mbalimbali kutoka kwenye kundi hilo na kuhamia kwengine.

Moja wa watu waliotoka ni Khadija Yusuph ambaye kwa sasa yupo kwenye kundi la Wakali Wao Modern Taarabu chini ya Thabiti Abduli.

Akizungumzia mkanganyiko huo, Khadija  ambaye aliwahi kutamba na nyimbo mbalimbali kama ‘Zibeni Njia Si Riziki Yake, anasema kuwa msanii hana kambi ya kudumu.

“Jahazi limevunjwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwa Mzee Yusuf wakati anaacha muziki alisema hatavunja kundi hilo, lakini Mungu mwenyewe ndo atalivunja na tayari dua yake imepokelewa na Mungu,” anasema.

Pia Khadija amesema furaha ya kaka yake Mzee Yusuf imekamilika kwa sasa na dua zake pia zitakuwa zimepokelewa na Mungu kama alivyokuwa akiomba kwamba ifikie kipindi hata nyimbo zake zisiwe zinapigwa.

Asichosahau kamwe

Akizungumzia suala ambalo hatalisahau toka ameanza fani hiyo ya uimbaji, Khadija anasema kuwa ni kutendo cha kutukanwa mitandaoni na kusababisha kujiondoa kwenye mitandao hiyo kwa muda.

“Yaani nimekutana na changamoto nyingi toka nianze kuimba, ila hii ya mtu anatukana mtandaoni alafu naambiwa mimi nimewatuma imeniumiza sana na kamwe sitasahau,” anasema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -