Thursday, December 3, 2020

Kuichunguza simu ya mpenzi wako ni ulimbukeni?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA MICHAEL MAURUS (michietz@yahoo.com, 0713556022)

KARIBUNI ndugu wasomaji katika safu hii ya uhusiano wa kimapenzi ambayo itakuwa ikiwajia kila Jumamosi na Jumanne katika ukurasa huu, ikitoa nafasi kwenu kufahamu na kuchangia mambo mbalimbali yahusianayo na mapenzi.

Mada yetu ya leo ni ile ambayo imekuwa ikiwatesa wengi na wakati mwingine kutikisa uhusiano wa wapendanao ambayo si nyingine, bali suala zima la simu za mkononi zinavyowatia majaribuni wenza.

Ni ukweli usiopingika kuwa, simu zimekuwa ni moja ya njia rahisi ya mawasiliano baina ya mtu na mtu, japo wakati mwingine, wapo ambao wamekuwa wakizitumia vibaya na mwisho wa siku kuwa sumu ndani ya wawili waliopendana.

Lakini ili simu igeuke kuwa sumu, itategemea na mhusika anavyoitumia, hasa anapokuwa na mwenza wake.

Kuna siku nikiwa katika moja ya daladala jijini Dar es Salaam, kuna abiria wawili waliokaa katika siti moja ambao walikuwa wakijadiliana jambo ambalo lilinivutia na kuona ni vema nikalileta kwenu kupitia safu hii.

Abiria wale ambao ni wasichana, mmoja alikuwa akimsimulia mwenzake tabia ya mpenzi wake kumzuia kupokea wala kuigusa simu yake.

Binti yule alikuwa akisema kuwa, pamoja na kuamini kuwa anapendwa mno na mpenzi wake huyo, lakini wakati mwingine anapatwa na wasiwasi juu ya penzi lao hilo kutokana na tabia ya mpenzi wake.

Alisema kuwa hata wawe na furaha kiasi gani na mpenzi wake huyo, anapoigusa simu yake tu furaha hiyo hutoweka ghafla na kuwa ugomvi unaoishia kwa mpenzi wake kuondoka katika eneo walilokuwapo au hata wakati mwingine kumpiga.

Kwa bahati mbaya kwangu, wakati mazungumzo yao ambayo yalinivutia mno yakiendelea, daladala lile lilifika katika kituo nilichotaka kushuka. Ilinibidi nishuke japo nilipenda kuendelea kusikiliza stori za wawili wale.

Ndugu wasomaji, katika uhusiano wa kimapenzi baina ya wawili wapendanao, hali kama iliyokuwa ikielezewa na abiria yule, imekuwa ikitokea kwa baadhi ya wapenzi.

Wapo ambao hali hiyo imekuwa ni ya kawaida, huku kila mmoja akikubaliana nayo, lakini wengine imekuwa ikiwaumiza mno.

Unapowauliza wale ambao wanakubaliana nayo hali hiyo, huwa wanadai kuwa kupokea au hata kuchunguza simu ya mpenzi wako ni ushamba na si ustaarabu.

Pia, wapo wanaodai kuwa, tabia ya kupokea au kuchunguza simu ya mpenzi wako inatokana na wivu wa kijinga na pia tabia hiyo inaonyesha jinsi mtu asivyomwamini mpenzi wake.

Lakini hebu kila mmoja wetu ajiulize, iwapo unampenda kwa dhati mpenzi wako, utajisikiaje iwapo ukiigusa simu yake atakurukia na kukunyang’anya?

 

Au je, utajisikia vipi iwapo mpenzi wako anapokwenda bafuni anabeba simu yake au anaizima na kuifunga na baada ya kutoka huko ndiyo anaiwasha kama anavyofanya usiku wakati wa kulala?

Lakini je, utajisikiaje pale unapokuwa na mpenzi wako, simu yake ikiita tu anaizima au kutoka nje fasta kwenda kuipokea huko?

Hebu nitoe fursa kwa wasomaji wa safu hii kuchangia mada hii juu ya suala zima la iwapo ni ulimbukeni au ushamba kuigusa au kuchunguza simu ya mpenzi wako unayempenda kwa dhati ambaye hupo tayari kumuona akipotea kwa kudanganywa na matapeli wa mapenzi ambao wamekuwa wakibuni mbinu za kuwalaghai wapenzi wa wenzao. Maoni yenu hayo nitayachapisha katika toleo la Jumanne ya wiki ijayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -