Saturday, October 31, 2020

KUIGUSA SIMU YA MPENZI WAKO NI ULIMBUKENI?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MICHAEL MAURUS (michietz@yahoo.com, 0713556022/0783 324232)

KARIBUNI ndugu wasomaji katika safu hii ya uhusiano wa kimapenzi ambayo huwa inawajia kila Jumanne na Jumamosi, ikitoa nafasi kwenu kufahamu na kuchangia mambo mbalimbali yahusianayo na mapenzi.

Awali ya yote, nitoe shukrani zangu za dhati kwa wote ambao walichangia mada zilizopita.

Jumanne tuliendelea na mada iliyohusiana na sababu za kuvunjika kwa uchumba au uhusiano wa kimapenzi baina ya wawili waliopendana.

Kati ya wasomaji wa safu hii, yupo aliyenipigia simu akielezea jinsi anavyokerwa na mpenzi wake kumzuia kuigusa simu yake.

Msomaji huyo aliyependa kutambulishwa kwa jina moja la Omari wa Dar es Salaam, alisema kuwa mpenzi wake huyo anapokuwa nyumbani simu yake hupenda kuificha na akilala huizima kabisa na anapohoji, mwenzake huyo huja juu na wakati mwingine kuibuka kwa ugomvi baina yao.

Hivyo Omari aliuliza afanye nini kutokana na hali hiyo?

Kutokana na kisa hicho, nimeona ni vema kuirudia moja ya mada zilizopita ambayo naamini itawagusa wengi.

Mada hiyo si nyingine bali ni ile inayosomeka kwa kichwa ‘Kuigusa simu ya mpenzi wako ni ulimbukeni?

Ndugu msomaji, simu zimekuwa ni moja ya njia rahisi ya mawasiliano baina ya mtu na mtu, japo wakati mwingine, wapo ambao wamekuwa wakizitumia vibaya na mwisho wa siku kuwa sumu ndani ya wawili waliopendana.

Lakini ili simu igeuke kuwa sumu, itategemea na mhusika anavyoitumia, hasa anapokuwa na mwenza wake.

Katika uhusiano wa kimapenzi baina ya wawili wapendanao, kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara inayosababishwa na simu.

Kutokana na hali hiyo, wapo ambao mwisho wa siku wameamua kutozigusa simu za wapenzi wao ili kuepusha shari baina yao.

Wapo ambao hali hiyo imekuwa ni ya kawaida, huku kila mmoja akikubaliana nayo, lakini wengine imekuwa ikiwaumiza mno.

Unapowauliza wale ambao wanakubaliana nayo hali hiyo, huwa wanadai kuwa kupokea au hata kuchunguza simu ya mpenzi wako ni ushamba na si ustaarabu.

Pia, wapo wanaodai kuwa tabia ya kupokea au kuchunguza simu ya mpenzi wako inatokana na wivu wa kijinga na pia tabia hiyo inaonyesha jinsi mtu asivyomwamini mpenzi wake.

Lakini hebu kila mmoja wetu ajiulize, iwapo unampenda kwa dhati mpenzi wako, utajisikiaje iwapo ukiigusa simu yake atakurukia na kukunyang’anya?

Au je, utajisikia vipi iwapo mpenzi wako anapokwenda bafuni anabeba simu yake au anaizima na kuifunga na baada ya kutoka huko ndiyo anaiwasha kama anavyofanya usiku wakati wa kulala?

Lakini je, utajisikiaje pale unapokuwa na mpenzi wako, simu yake ikiita tu anaizima au kutoka nje fasta kwenda kuipokea huko?

Hebu nitoe fursa kwa wasomaji wa safu hii kuchangia mada hii juu ya suala zima la iwapo ni ulimbukeni au ushamba kuigusa au kuchunguza simu ya mpenzi wako unayempenda kwa dhati ambaye haupo tayari kumwona akipotea kwa kudanganywa na matapeli wa mapenzi ambao kila siku ya Mungu wamekuwa wakibuni mbinu za kuwalaghai wapenzi wa wenzao.

Tukutane Jumanne ya wiki ijayo. Ahsanteni sana na nawatakia heri ya Mwaka Mpya.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -