Sunday, January 17, 2021

KUMBE ARSENAL WANA JESHI LIGI YA MABINGWA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON,England

MSIMU huu timu ya  Arsenal haitashiriki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwa 1997.

Hii ni kutokana na kwamba, Gunners walishindwa kufuzu michuano hiyo baada ya kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita.

Kwa kushika nafasi hiyo msimu huu, kocha wao,  Arsene Wenger, atakiongoza kikosi hicho kwenye michuano ya Ligi ya  Europa.

Kwa kushindwa kushiriki kwenye michuano hiyo, inaonekana kuwa pengine kuwaumiza baadhi ya mashabiki  wa Gunners, kutokana na ukweli kwamba ni kitu ambacho hawakukitarajia na pengine hawakipendi.

Hata hivyo, pamoja na kuwa katika hali hiyo, kuna baadhi yao ambao pengine watakuwa wakifarijika na huku wakijiona timu hiyo inashiriki michuano hiyo kiaina kutokana na kuwapo nyota wao saba ambao wanachezea klabu mbalimbali zinazoshiriki kwenye michuano hiyo.

Mastaa hao saba ambao pengine wanaweza kuwaondolea upweke wa kukosekana kikosi chao ni kama ifuatavyo:

Wojciech Szczesny (Juventus)

Licha ya Juventus kumtegemea sana staa wao, Gianluigi Buffon, lakini raia huyo wa Poland anaweza kuwa akimsaidia kutokana na uwezo aliouonesha tangu alipojiunga na  Juventus akitokea  Gunners majira haya ya joto, ikiwa ni baada ya kucheza kwa mkopo katika klabu ya AS  Roma.

Hata hivyo, licha ya mechi za hatua ya makundi kuwa chache, lakini mzuia mashuti huyo anaweza kudaka mechi walau moja ama mbili endapo Juventus itafanikiwa kufuzu hatua hiyo.

Thomas Vermaelen (Barcelona)

Baada ya kutua Barca  msimu uliopita akitokea AS  Roma, beki huyo  raia wa Ubelgiji ametajwa kwenye kikosi cha vinara hao wa  Catalans kitakachoshiriki kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Akiwa ameshajijengea jina katika kipindi alichokuwa akikipiga kwenye klabu hiyo ya  Emirates, alijikuta akikumbwa na majeraha, lakini bado akawa anatumika kwenye kikosi cha timu ya taifa lake.

Cesc Fabregas (Chelsea)

Licha ya kuwa hajawahi kutwaa ubingwa wa michuano hiyo tangu alipoondoka Arsenal na kurejea Barcelona mwaka 2011 kwa ajili ya kusaka mataji zaidi, lakini baada ya kufanya vizuri katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia na za Mataifa ya Ulaya kulimwongezea sifa kiungo huyo.

Usiku wa kuamkia jana Fabregas alikuwamo kwenye kikosi cha Chelsea kilichoinyuka kwa mabao 6-0 Qarabag na huku akitoa mchango wa hali ya juu kiasi ambacho kinaweza kuwapa faraja mashabiki wa Arsenal ambao alikuwa kipenzi chao.

Alex Oxlade-Chamberlain (Liverpool)

Kwa kuitema Arsenal na kwenda kujiunga na  Liverpool majira haya ya joto, kiungo huyo wa timu ya Taifa ya  England ina maana ameikacha Ligi ya  Europa  na kwenda kushiriki kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Akiwa na Gunners misimu ya hivi karibuni amekuwa akiishia mara kwa mara katika raundi ya pili, lakini sasa huenda ana matumaini ya kupiga hatua nyingine moja mbele akiwa na  Reds.

Ovie Ejaria (Liverpool)

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka  19, aliruhusiwa na Arsenal  kuondoka kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Hata hivyo, baada ya kuruhusiwa msimu uliopita aliweza kucheza mechi tisa za kikosi cha kwanza za Liverpool na alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya England kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20.

Licha ya kuwa pengine vita ya kugombea nafasi katika safu ya kiungo inaweza kuwa kubwa, lakini  kocha wao, Jurgen Klopp, ameshaonesha wazi kutohofia kuwapa nafasi makinda na hivyo pengine staa huyo akapewa nafasi zaidi kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Oguzhan Ozyakup (Besiktas)

Mzaliwa huyo wa Uholanzi anayechezea timu ya Taifa ya Uturuki, alikuwa kwenye vitabu vya  Arsenal  kwa kipindi cha miaka minne na alikuwa kwenye benchi wakati wa mchezo ambao walifungwa na Manchester United mabao  8-2 mwaka 2011.

Baada ya kipigo hicho, wiki chache baadaye aliweza kucheza mchezo mmoja ambao ndio ulikuwa pekee kwake kuichezea Gunners, ukiwa ni wa michuano ya Kombe la Ligi dhidi ya  Shrewsbury.

Hata hivyo, baada ya kuondoka na kwenda kujiunga na  Besiktas majira ya joto yaliyofuata, staa huyo alianza kuonekana kuwa tegemeo kwenye klabu hiyo ya  Istanbul  na ameiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi mara mbili na huku akichezea timu ya taifa mechi 25.

Chris Willock (Benfica)

Tangu ajiunge na Arsenal akiwa na umri wa miaka mitano, kinda huyo raia wa Uingereza, Willock, aliweza kupanda na kisha akafanikiwa kucheza kwenye kikosi cha kwanza wakati wa mechi ya Kombe la Ligi  dhidi ya  Nottingham Forest  mwaka mmoja uliopita.

Hata hivyo, tatizo la kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara ndilo lililomfanya majira haya ya joto atimkie  Benfica na licha ya kuwa hayupo kwenye kikosi cha vinara hao wa Ureno ambao watashiriki hatua hii ya makundi, lakini pengine anaweza kulazimisha kuwamo kwenye kikosi hicho kama wataweza kutinga hatua ya mtoano.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -