Saturday, November 28, 2020

KUMBE DE GEA HAYUPO TATU BORA YA MAKIPA LIGI KUU ENGLAND?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

MLINDA mlango wa Manchester United,

David de Gea na Hugo Lloris wa Tottenham wamekuwa wakisifiwa sana kwa kazi wanayoifanya na mwishoni mwa wiki hii watakuwa watu muhimu wakati timu zao zinakutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England katika Uwanja wa Old Trafford.

Lakini kwa mujibu wa mtandao wa takwimu wa Opta, kuna makipa wengine wamewazidi wawili hao Ligi Kuu England katika msimu huu.

Kwa kila shuti lililopigwa Ligi Kuu England, mtandao wa Opta umeweka viwango kulingana na sababu mbalimbali kama eneo na umbali lilipopigwa shuti hilo.

Kila shuti limepewa alama yake kuanzia sifuri hadi 1.00. Ambapo ikiwa shuti limepewa alama alama ya 0.5, ina maana asilimia 50 mpigaji wa shuti alikuwa na nafasi ya kufungwa.

Kwa kutumia njia hiyo wameweza kujumlisha jumla ya mabao ambayo timu moja ingeweza kuifunga nyingine kwenye mechi.

Kujumlisha alama hizo zinasaidia kupata ambao wameokoa mashuti ambayo yalikuwa ni mabao ya wazi na nani ameruhusu mabao rahisi.

Kwa njia hiyo, mlinda mlango wa Burnley, Tom Heaton anaingoza kwa orodha ya makipa bora msimu huu. Nyota huyo wa England angekuwa ameruhusu mabao 24 kwa mujibu wa takwimu za mtandao wa Opta, lakini ameweza kuruhusu mabao 19 pekee. Baada ya kuokoa mashuti 64 kati ya 83 yaliyopigwa langoni mwake na timu pinzani na kumfanya wastani wake wa kuokoa mashuti kuwa asilimi 77.1.

Lee Grant wa Stoke City anashika nafasi ya pili kwa ubora. Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 33, alijipata sifa sana kwa kiwango chake alichoonyesha katika mechi dhidi ya Manchester United, ambayo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 akiwa ameruhusu mabao matano kati ya nane aliyotarajiwa kufungwa.

Nafasi ya tatu ni mlinda mlango wa Arsenal, Petr Cech, ambaye angekuwa amefungwa mabao 16, lakini kwa mujibu wa mtandao wa Opta, amefungwa mabao 14 kati ya hayo 16.

Mlinda mlango wa Tottenham, Lloris ameruhusu mabao tisa katika nafasi 10 alizotarajiwa kufungwa, hivyo anashika nafasi ya nne.

Kipa wa Hispania, De Gea alitarajiwa kuwa awe ameruhusu mabao chini ya 15, lakini Opta wanasema ameruhusu mabao 16. Hiyo ina maana amefanya makosa na kuwaruhusu washambuliaji kupasia kwenye nyavu zake.

Mlinda mlango wa Hull City, David Marshall ana rekodi mbaya zaidi ya De Gea, ambapo Opta wanasema timu hiyo ilipaswa kuwa iwe imefungwa mabao 14 lakini badala yake amefungwa mabao 22.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -