Monday, January 18, 2021

KUMBE DRAKE ANATOKA NA J-LO ILI AMTIBUE P. DIDDY!

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LOS ANGELES, Marekani

ZIKIWA zimebaki siku chache kabla ya kumalizika kwa mwaka 2016, wadau wa burudani nchini Marekani walishuhudia bonge la filamu.

Hapa sizungumzii maigizo, bali hakuna unavyoweza kutofautisha uhusiano wa kimapenzi kati ya mastaa Jeniffer Lopez ‘J-Lo’ na Drake na filamu.

J-Lo ana umri wa miaka 47, huku Drake akiwa ndio kwanza ana umri wa miaka 30. Na mapenzi yao yalianza kuonekana hadharani kupitia mitandao ya kijamii na hiyo ilikuwa ni Desemba 27.

Fununu za wawili hao kuwa mwili mmoja zilianza kuvuma baada ya Drake kuonekana mara mbili kwenye matamasha mawili ya mwimbaji J-LO yaliyofanyika jijini Las Vegas.

Hata hivyo, tatizo si tofauti ya umri wao, bali kuna sababu nyingi ambazo zimeufanya uhusiano wao kuwa gumzo kwenye vyombo vya habari nchini Marekani na duniani kote.

Kuna madai kuwa kuna siri nzito ya wawili hao kuwa pamoja, ikiwamo suala la kulipiza kisasi. Ngoja nikwambie.

Imeelezwa kuwa lengo la Drake kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na J- Lo, ni kulipiza kisasi kwa hasimu wake mkubwa katika biashara ya muziki, Sean ‘Diddy’ Combs au P. Diddy kama anavyofahamika na wengi.

Madai hayo yameibuliwa na mtangazaji mmoja wa kituo cha redio anayefahamika kwa jina la Funkmaster Flex.

Flex anaamini kuwa wala Drake hana mapenzi ya dhati na mwanamama huyo ila lengo lake ni kuibua uhasama aliokuwa nao na P. Diddy.

Ikumbukwe kuwa kwa miaka mingi kumekuwa na vita kubwa kati ya washikaji hao, Drake na P. Diddy na mwaka 2014 waliwahi kushikana mashati katika klabu moja ya usiku jijini Las Vegas.

Lakini pia, P. Diddy aliwahi kutoka na  J-Lo kwa miaka kadhaa kabla ya kubwagana mwishoni mwa mwaka 1999.

Mastaa hao waliachana baada ya tukio la P. Diddy kutumia bastola akiwa kwenye ukumbi wa usiku ambapo alijeruhi watu watatu.

Mtangazaji Flex anasema kitendo cha Drake kutoka na J-Lo kinaashiria kuwa anataka kumchokoza adui wake P. Diddy.

Flex ameongeza kuwa Diddy ni ‘bwana mdogo’ na hana hadhi ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na J-Lo. Flex amesema labda Drake anatafuta ‘kiki’ tu.

Ukiachana na Flex, kwa upande mwingine, mwanamuziki Rihanna ambaye aliwahi ‘kubanjuka’ na Drake,  hajafurahishwa na uhusiano wa mpenzi wake huyo wa zamani na J-Lo.

Baada ya kusikia taarifa kuwa mpenzi wake huyo wa zamani ana uhusiano na J-LO, Rihanna ameamua kuwapotezea wote wawili kwenye mitandao ya kijamii na wala hataki stori nao.

Wakati wa Sikuu ya Krismasi, akiwa mapumzikoni kwenye visiwa vya Barbados ambako ndiko alikozaliwa, Rihanna aliacha kuwa mfuasi ‘follower’ wa J-LO kwenye mtandao wa Instagram.

Kabla ya tifu hilo, Rihanna mwenye umri wa miaka 28, alikuwa swahiba mkubwa wa J-Lo na mara kwa mara walionekana kwenye hafla mbalimbali.

Wafuatiliaji wa masula ya burudani watakumbuka kuwa mwanzoni mwa mwaka 2016, Rihanna aliwahi kumpa J-Lo zawadi ya viatu ambavyo hupatikana kwenye kampuni yake ya mavazi.

Kwa upande wake, Rihanna ametajwa kuwa mbioni kumsaka mwenza ikiwa ni katika kulipiza kisasi cha J-Lo kumchukua Drake.

Imeelezwa kuwa mwanadada huyo anataka kuipumzisha akili yake kutokana na mapenzi ya wawili hao na lengo lake ni kuuanza mwaka huu akiwa mpya.

“Ni mwaka mpya (2017) na katika hilo, Rihanna anataka kuwa mwanamke mpya.

“Hataki kukutana na majanga mengine kama hayo. Amechoka kuumizwa na wanaume ambao wamekuwa wakiigiza kumpenda huku vitendo vyao vikiwa tofauti. Hakuna nafasi nyingine kwa wanaume wapuuzi. Ya kale yamepita na sasa ni wakati wa yajayo,” kilisema chanzo kimoja cha habari kilipokuwa kikihojiwa na mtandao wa HollywoodLife.com.

Mrembo huyo aliwahi kuumizwa kimapenzi na aliwahi kutoka kimapenzi na staa mwenzake Cris Brown, lakini waliachana kabla ya kuangukia kwenye mikono ya Drake naye amemtema hivi karibuni.

Mbali na washikaji hao, Rihanna ana orodha ndefu ya wanaume aliowahi kutajwa kupumzisha nao akili wakiwamo Leonardo DiCaprio, Justin Timberlake, Jay-Z na mastaa wa mpira wa kikapu J. R. Smith na Rashard Lewis.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -