Friday, October 30, 2020

KUMBE HAJASAINI… MENEJA WA TSHABALALA AFUNGUKA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR

MENEJA wa beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Heri Mzozo, amefunguka na kudai kuwa mchezaji wake huyo bado hajasaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo ya Msimbazi.

Akizungumza na BINGWA jana, Heri Mzozo alifunguka na kuweka wazi kila kitu kuhusiana na Tshabalala kusaini mkataba mpya ndani ya Simba.

“Kimsingi Tshabalala bado hajasaini mkataba wowote na Simba mpaka dakika hii ninapozungumza na wewe, hadi tulipofika hapa sisi tumewaachia viongozi Simba kuamua wafanye nini, maana wao ndio wenye uamuzi wa mwisho kama wanatimiza matakwa yetu au la,” alisema Mzozo.

Alisema kwa upande wake, yeye kama meneja anasubiri viongozi wa Simba kumaliza shughuli za kutafuta fedha kiasi cha Sh milioni 60 ambazo Tshabalala anazitaka ndipo zoezi la kusaini mkataba mpya lifanyike.

“Kimsingi Tshabalala ataendelea kubaki Simba, kwa maana tumekaa na viongozi wa Simba na kufanya nao mazungumzo ya kina, hivi sasa wanahangaika kupata hizo fedha ili tuweze kusaini huo mkataba,” alisema Mzozo.

Katika hatua nyingine, Mzozo alisema ameamua kumshawishi Tshabalala kubaki Simba ili aweze kuendelea kupata uzoefu zaidi kuliko kuondoka na kujiunga na klabu nyingine hapa nchini.

“Ngoja nikwambie ukweli tu uelewe ni hivi, Tshabalala hawezi kwenda timu nyingine kwa maana anaweza kupoteza kipaji chake kutokana na presha ya timu hiyo na mashabiki wake sasa, ngoja aendelee kubaki hapa kwa miaka mingine miwili ataondoka,” alisema Mzozo.

Licha ya Mzozo kuendelea kukanusha taarifa za kuwa Yanga inamfukuzia staa huyo, lakini BINGWA limepata tetesi kuwa klabu hiyo ya Msimbazi imeweka mezani dau la Sh milioni 80, ambalo linaonekana kuanza kumvuruga mtu mmoja wa karibu na beki huyo ambaye sasa anatumia ushawishi wa hali ya juu kuhakikisha anaenda kudaka fedha hizo ambazo ni nyingi sana, ukilinganisha na zile zinazotarajiwa kutolewa na Simba.

Inaaminika ili kupambana na nguvu ya fedha ya Yanga, hadi mfadhili wa zamani wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘MO’, ametia mkono wake katika kuhakikisha Tshabalala haendi Jangwani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -