NA JESSCA NANGAWE
MASHABIKI wa Bongo Fleva wanamtambua msanii kutoka kundi la Wasafi, Harmonize kutokana na kipaji chake cha kuimba tu, lakini kumbe jamaa pia ni mkali sana kwenye soka.
Akizungumza na DIMBA, Harmonize alisema, amekuwa shabiki mkubwa wa mpira wa miguu na mbali ya ushabiki, ana uwezo mkubwa kucheza, ukiachilia mbali kuimba.
“Watu wananitambua kama msanii tu, lakini nataka mashabiki wajue kama mimi naumiliki mpira vilivyo…nilikuwa sikosi mechi za ndondo uswahilini kabla muziki haujanikolea na hata nikiitwa kuichezea Majimaji ama Ndanda nipo tayari, kwa kuwa pia ni mtu wa mazoezi sana,” alisema Harmonize.
Alisema muda mwingi amekuwa akitumia kufanya mazoezi ili kuweka mwili wake sawa.