Wednesday, October 28, 2020

KUMBE HAZARD CHA MTOTO KWA DEMBELE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England


MSIMU huu winga wa Chelsea, Eden Hazard, ameonekana kufurahia maisha ndani ya klabu hiyo akiwa na mchango mkubwa hadi klabu hiyo kuongoza msimamo wa Ligi Kuu England.

Mbelgiji huyo hadi sasa amepachika mabao tisa ndani ya mechi 17 za ligi na ni mmoja wa wanaotabiriwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya PFA.

Moja ya uwezo unaomfanya Hazard aogopeke na mabeki wa timu pinzani ni namna anavyoweza kupangua ngome kwa ukokotaji mpira kwa kasi na ukisema umtaje kuwa ni bora kwenye hilo ndani ya ligi tano kubwa za Ulaya hautakosea.

Lakini katika suala la kukokota mpira na ukafaniwa kutengeneza nafasi, kutoa pasi au kufunga, Hazard amepitwa na wachezaji mbalimbali waliofanya vyema mwaka huu 2016.

Winga hatari wa Borussia Dortmund, Ousmane Dembele, anaongoza kwa kukokota mpira mara 144 na kufanikiwa katika ‘misheni’ hiyo huku anayekamata nafasi ya pili akiwa ni winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha (141) na mshambuliaji hatari wa Barcelona, Neymar akifanikiwa kukokota mpira mara 138.

Kwenye orodha hiyo, Hazard amekamata nafasi ya nne akifanikiwa kukokota mara 118, huku winga wa PSG, Hatem Ben Arfa, akiwa nafasi ya tano (115).

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -