Tuesday, November 24, 2020

KUMBE KIBOKO YA SIMBA NI PLUIJM

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ONESMO KAPINGA

GOoooo… ni Kichuya tena. Lilikuwa ni bao la ushindi la Simba katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya watani wao Yanga, uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Shangwe ililipuka baada ya Simba kujihakikishia ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa katika mchezo huo, ambao ulikuwa ni muhimu kwa kila timu ili kujiweka katika mazingira bora zaidi ya kutwaa ubingwa wa msimu huu.

Bao la Shiza Ramadhan Kichuya lilikoleza furaha zaidi baada ya mashabiki wa Simba kunyamazishwa dakika ya tano kabla ya Laudit Mavugo kusawazisha kufuatia Yanga kutangulia kufunga bao kwa penalti iliyofungwa na Simon Msuva.

Kwa muda mrefu mashabiki wa Simba walionekana kukosa raha, baada ya kufungwa bao hilo kufuatia maandalizi kabambe waliyofanya kabla ya mchezo huo, lakini Kichuya aliibua shangwe kubwa kwa kufunga bao la ushindi.

Kichuya alionekana kama ni mchawi wa Yanga baada ya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo kufunga bao zuri wakati Simba wakiwa nyuma ya bao 1-0.

 

Simba ikiongozwa na kocha mkuu Mcameroon Joseph Omog, pengine naweza kusema ni kocha mwenye akili nyingi sana, kutokana na kupanga kikosi chake vizuri kilichokuwa kikicheza pungufu kufuatia mwamuzi wa mchezo huo, Mathew Akram kumwonyesha kadi nyekundu Janvier Bokungu.

Hapo ndipo ninamwona Omog ni fundi kutokana na jinsi alivyoziba pengo la Bukungu na kumrudisha kiungo wa timu hiyo, Muzamiru Yassin.

Haikutegemewa kama Omog angeweza kufanya mabadiliko kama haya, hasa ukizingatia Yanga walikuwa katika presha ya kutaka kushinda ili waweze kujiweka katika mazingira bora zaidi ya kutetea ubingwa wao.

Lakini kitendo cha kuwaweka wachezaji muhimu benchi kama Said Ndemla, Jonas Mkude na Kichuya, zilikuwa ni mbinu za Omog na kama alijua angewaanzisha mapema wangeweza kupewa kadi nyekundu na kuharibu mipango yake ya ushindi.

Omog ni kama aliusoma mchezo wa kwanza uliochezwa Oktoba mosi mwaka jana, ambapo Mkude alionyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi waliyechezeshwa pambano hilo, Martin Saanya na kuvuruga kabisa mipango yake ya ushindi, wakati timu hizo zilizotoka sare ya kufunga bao 1-1.

Mcameroon huyo alikuwa na sababu zake zilizowafanya akina Mkude kuanzia benchi na pengine mipango yake ilikamilika, baada ya Bokungu kuonyesha kadi na baadaye kufanya mabadiliko ambayo yalionekana kwenda na mipango yake.

Nikirudi kwa kocha wa Yanga, Mzambia George Lwandamina, naweza kusema kwamba aliingilia na mbinu zilizoeleka na pengine inatokana na ugeni wake katika timu hiyo.

Pamoja na kwamba Lwandamina alikuwapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa Oktoba mosi mwaka jana, lakini Hans van der Pluijm alikuwa bado ni kocha mkuu wa Yanga.

Pluijm ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa ufundi wa Yanga baada ya kumpisha Lwandamina, naamini yeye ni kiboko wa Simba kutokana na rekodi yake.

Yanga ya Pluijm ilikuwa inaipa shida Simba, naamini hivyo kutokana na wastani nzuri wa kuifunga Simba, lakini nitaendelea kuamini kwamba Mholanzi huyo ni kiboko ya Msimbazi.

Sikuwa na nafasi yoyote ya kuweza kuwashauri Yanga juu ya mabadiliko yaliyofanywa katika benchi la ufundi, nikiamini kwamba bado Pluijm alikuwa ana uwezo wa kuifikisha mbali timu hiyo kwenye michuano ya ndani ya kimataifa.

Nguvu ya Pluijm ilihitajika katika kuhakikisha Yanga inaibuka na ushindi juzi, ingawa sifahamu kama Lwandamina alimshirikisha kwa namna gani kocha aliyemtangulia.

kapssmo@gmail.com 0716985381

Tukutane Jumatatu ijayo

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -