Thursday, October 29, 2020

Kumbe kuna sayari inaitwa Wenger

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

Arsene Wenger wiki hii amefikisha miaka 20 katika klabu ya Arsenal.

Baada ya mambo yote kwenye soka la England, unaweza ukafikiria unamjua ‘Le Professeur’.

Kocha huyo Mfaransa amekuwa akiishi maisha yake kwa siri sana na mambo yaliyotokea zamani yamesahaulika.

Hivyo kuna mambo 20 katika miaka 20 ya kocha huyo kwenye klabu ya Arsenal ambayo huyajui.

 

 1. Arsene Wenger alipata kazi kama zari, baada ya mwaka 1989 kwenda kuangalia mechi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Highbury, alikutana na makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, David Dein na kupata muda mwingi wa kuzungumza na Wenger, ambaye wakati huo hakuwa akiweza kuzungumza Kiingereza vizuri, alikuwa kama anaigiza.
 1. Aliacha shughuli za siku ya mwisho za usajili wa kiangazi mwaka 2014 na kwenda Vatican kukutana na Papa Francis.
 1. Badala ya kuangalia mechi nyumbani kwao Strasbourg nchini Ufaransa alikozaliwa, alikuwa anavuka boda kwenye Ujerumani na safari zake zilikuwa kwenda kuiona Borussia Monchengladbach.
 1. Wenger alibadilisha mlo kwa wachezaji wa Arsenal, hasa matumizi ya nyama na badiliko la afya na kusababisha Ian Wright kulalamika kuwa kila kitu ni mboga za majani.
 1. Ana shahada ya uzamili katika masuala ya uchumi, aliyosomea Chuo cha Strasbourg.
 1. Wenger hajawahi kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini pia hajawahi kubeba Kombe la Ligi pamoja na kucheza fainali mwaka 2007 dhidi ya Chelsea pamoja na Birmingham mwaka 2011.
 1. Ana tatizo la kujali muda, Mfaransa huyo anajulikana kwa tabia yake ya kuchelewa kwenye mikutano ya waandishi wa habari, wiki iliyopita alichelewa saa nne kutoka kwenye muda wa kikao cha kuzungumzia safari yake ya Hull City.
 1. Wenger ni shabiki mkubwa wa marehemu Bob Marley, hasa anavutiwa na maisha yake kwa kuwa hakuwa akiishi kwa kuigiza.
 1. Haendi kunywa mvinyo akialikwa baada ya mechi na Sir Alex Ferguson aliwahi kusema ni kocha pekee ambaye hafanyi hiyo, lakini alimshauri afuate tamaduni hizo.
 1. Anazungumza lugha sita, Kifaransa, Kijerumani, Kiingereza, Kihispania, Kiitaliano na Kijapani kidogo. Alikuwa akizungumza Kifaransa pekee, lakini akiwa na miaka 29 alikwenda kujifunza Kiingereza nchini England katika Chuo cha Cambridge.
 1. Alikuwa kocha wa kwanza asiyetokea England kunyakua taji la Ligi Kuu England.
 1. Wazazi wake walikuwa wanamiliki mgahawa na duka la spea za magari.
 1. Alianza kucheza soka lake la kulipwa akiwa na umri wa miaka 29 kwa mara ya kwanza kwenye timu ya RC Strasbourg na kufanya hivyo kwa miaka 12.
 1. Mechi yake ya kwanza kuishuhudia Arsenal, walishinda mabao 2-0 dhidi ya Tottenham na mchezaji aliyemvutia sana mwaka huo 1989, alikuwa ni Perry Groves.
 1. Wenger alianza ukocha na umri wa miaka 33 na alikuwa mgonjwa na aliishusha daraja klabu yake ya kwanza ya Nancy-Lorraine.
 1. Wenger ana sayari inayojulikana kwa jina lake. Sayari hiyo iligundulika Machi 29, 1998 na Ian P. Griffin, ambaye ni shabiki wa Gunners. Hiyo sayari inaitwa 33179 Arsenewenger.

17. Ni kocha mwenye hasira na amewahi kugombana na Ferguson baada ya kumfokeoa Ruud van Nistelrooy.

 1. Wenger na mke wake wa zamani, Annie Brosterhous, ambaye alikuwa mchezaji wa mpira wa kikapu mwaka 2010, wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike na waliachana mwaka 2015.
 1. Mwaka 1997 aliandika kitabu cha Kijapani alichokiita ‘Roho ya Ushindi’, akizungumzia masuala ya soka la nchi hiyo.
 1. Wanyama anaowapenda sana ni mbwa na farasi.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -