Wednesday, October 28, 2020

KUMBE TATIZO SI DJUMA SIMBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWAMVITA MTANDA

*Siri nzito kutoka Rwanda yafichuka

*Yabainika Aussems alipenyezewa uzushi wa kumchukia Mrundi huyo kitambo

SIRI imevuja juu ya sababu za kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, huku ikidaiwa aliyekuwa bosi wake, Rayon Sports ya Rwanda, Ivan Minnaert, ndiye chanzo.

Habari zilizovuja juzi na jana kutoka Rwanda, zinadai kuwa wakati Djuma akiwa kocha msaidizi wa Rayon, bosi wake alikuwa ni Minnaert raia wa Ubelgiji.

Ilielezwa kuwa Mbelgiji huyo alipata dili la kuinoa AFC Leopard ya Kenya na kuiacha Rayon chini ya Djuma ambaye aliiwezesha timu hiyo ya Rwanda kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2016/17, huku wakiwa na mechi nne mkononi.

Mbali ya mafanikio hayo, Djuma pia aliiwezesha Rayon kuwachapa mabao 4-0 wapinzani wao wakubwa, APR, kabla ya kuwatambia tena katika mchezo wa fainali ya Peace Cup ambayo ni sawa na Kombe la FA hapa Tanzania na hivyo kuzima kabisa utawala wa wapinzani wao hao katika soka la Rwanda.

Kitendo hicho kiliwafanya mabosi wa timu yake hiyo kumpa mkataba wa miaka mitatu kama kocha mkuu.

Lakini kwa upande wa Minnaert, mambo yalimwendea kombo AFC Leopard na kutaka kurejea Rayon akitaka kuendelea kuwa juu ya Djuma.

Kitendo hicho hakikumfurahisha Djuma na kocha huyo kudaiwa kupinga hilo na hapo ndipo ‘bifu’ baina ya wawili hao lilipoanza.

Habari zaidi zinadai kuwa baada ya Minnaert kupata taarifa za ujio wa Patrick Aussems ndani ya kikosi cha Simba, aliwasiliana na Mbelgiji mwenzake huyo na kumchafua Djuma.

Imedaiwa kuwa kutokana na hilo, Aussems alianza kumchukia Djuma tangu wakiwa kambini Uturuki hadi waliporejea nchini na kuendeleza ‘bifu’ lake hadi alipofanikiwa kuwashawishi mabosi wa Simba na kuachana na Mrundi huyo kwa madai ya kile kilichoitwa ‘uswahili’ wake.

BINGWA lilimtafuta Djuma jana ili kuzungumzia madai hayo ambapo kocha huyo alijibu ‘kiutu uzima’ akisema, hakuwa na tatizo na Minnaert.

“Unajua linapotokea jambo utaona na mengine yanaibuka, lakini kwa upande wangu mpaka naondoka kule (Rayon), sikuwa na tatizo na mtu hata kwa kocha (Minnaert), sikuwa na shida naye, lakini katika kazi mambo ni mengi na chochote kinaweza kutokea,” alisema Djuma.

Kwa upande wake, Aussems alikataa kuzungumzia lolote kuhusiana na madai hayo, akisisitiza kazi kubwa iliyomleta Tanzania ni kuhakikisha anaisaidia timu yake kufanya vizuri.

“Sina taarifa kutoka kwa mtu kuhusiana na aliyekuwa kocha wangu msaidizi, hata hivyo sipendi kuzungumzia chochote juu yake,” alisema Aussems.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -