Sunday, November 29, 2020

KUMBE USHAURI WA CAPELLO NDIO UNAOMBEBA CONTE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

KWA sasa kocha wa Chelsea, Antonio Conte, ndiye habari ya mjini, baada ya kuiwezesha timu hiyo kucheza michezo 11 bila kufungwa.

Rekodi hiyo imekuja ikiwa ni baada ya msimu uliopita timu hiyo kufanya vibaya na huku ikiuanza msimu huu kwa kuchapwa na Liverpool na Arsenal.

Hata hivyo, baada ya kocha huyo kubadili mfumo na kuanza kutumia wa 3-4-3, timu hiyo inaonekana kuwa tishio  katika michuano ya Ligi Kuu England.

Hali hiyo imewafanya mashabiki wa kila  timu pamoja na makocha mbalimbali wa timu zinazoshiriki ligi hiyo kujiuliza kama ni mfumo wa kocha huyo unaompa mafanikio ama kuna kitu kingine.

Kutokana na maswali hayo kuwa mengi kocha huyo juzi aliamua kufunguka na kueleza siri ya mafanikio hayo akisema kuwa alipewa ushauri na Mwitaliano mwenzake, Fabio Capello, kuhusu changamoto zilizopo katika soka la England.

Katika mahojino na gazeti la Daily Mirror, kocha huyo anadai kwamba Mwitaliano huyo mwenzake ambaye ni kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya  England, alimweleza kuwa kukosekana kwa mapumziko ya majira ya baridi ndicho kitu kibaya katika soka la nchi hiyo na kimekuwa kikiziathiri pia timu za mataifa mbalimbali.

Kutokana na ushauri huo, Conte  ambaye alikuwa akinufaika na mapumziko ya majira ya baridi wakati akiinoa timu ya Taifa ya Italia anakiri akisema kwamba amekutana na mtihani mpya kucheza wakati wa kipindi cha Sikukuu za Krismasi, lakini anasema anachokiangalia ni kusonga mbele.

“Nakabiliwa na changamoto hiyo nikiwa hapa England na nimeshasikia mengi kutoka kwa makocha mbalimbali wakisema natakiwa kupumzika wakati wa majira haya ya baridi na zaidi ya yote ni kuhusu kuathirika kwa timu za  taifa,” anasema Conte.

Anasema, Capello mara zote alikuwa akimweleza kukosekana kwa mapumziko ya majira ya baridi kunaziathiri timu za taifa jambo ambalo linampa ugumu kujibu swali hilo.

“Ni vigumu kwangu kujibu kama ni kweli ama hapana kama kucheza wakati wa kipindi cha Krismasi ni tatizo. Lakini kwangu mimi hii ni mara ya kwanza kukutana na jambo hili ila najisikia  mwenye furaha kupata changamoto kama hii,” anasema Conte.

Conte anasema kufanya kazi katika sikukuu kama hii pia itakuwa ni changamoto ya kwanza kwa familia yake ambayo ilikuwa imezoea kupumzika wakati akizifundisha timu za Italia na Juventus.

“Mke wangu na binti yangu waliwasili hapa kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi nyumbani kwangu pamoja na kaka yangu na familia yangu, nadhani  ni kitu kizuri,” anasema Mwitaliano huyo.

Anasema itakuwa mara yao ya kwanza  kukutana na hali kama hiyo lakini itakuwa ni vizuri kwa yeye na timu yake kujipanga.

“Katika kipindi kama hiki tulikuwa tukikitumia kwa mapumziko. Wakati mwingine tulikuwa tukienda mjini  Lecce ama Torino na mara moja tulikwenda Dubai. Lakini jambo la muhimu ni kuwa na familia yangu wakati wa sikukuu ya Krismasi,” anasema kocha huyo.

Anasema kusherehekea sikukuu ya Krismasi na familia si jambo la muhimu bali ni kufikiria kuhusu mikakati ya kuisaidia timu yake ifanye vizuri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -