Monday, November 30, 2020

KUMBE WACHINA HAWANA HABARI NA BARCA, MESSI!

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

BEIJING, China

MANCHESTER United ndio klabu maarufu zaidi nchini China na sasa imewapiku mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich.

Timu tatu nyingine za Ligi Kuu England, Arsenal, Liverpool na Manchester City, zimetinga ‘top five’. Nafasi zinazofuata zimeshikwa na Real Madrid, AC Milan na Tottenham.

Barcelona inayotikisa Ulaya haifuatiliwi sana kwenye mitandao na mashabiki wa China, kwani ina idadi sawa na Borussia Dortmund na zinashika nafasi ya tisa.

Kwa upande wa wachezaji, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ndiye mchezaji anayefuatiliwa na mashabiki wengi wa soka China kupitia mitandao huku Mesut Ozil akiwa nyuma yake.

Cha kushangaza ni kwamba, Lionel Messi hayumo kabisa katika orodha ya wanasoka maarufu China, huku nafasi ya tatu ikienda kwa nyota wa kimataifa wa  Wales, Gareth Bale.

Hata hivyo, umaarufu huo ni wa mitandaoni, hivyo Man United ndiyo klabu inayofuatiliwa na mashabiki wengi wa soka kupitia teknolojia hiyo ya mitandao ya kijamii.

Ripoti hiyo imetolewa na Jarida la Red Card ambalo utafiti wake umeangalia ushawishi wa klabu 53 za Ulaya.

Red Card imepata takwimu hizo kutoka katika mitandao miwili ya China, WeChat na Weibo, pamoja na Twitter na Facebook.

Kwa mujibu wa Red Card, Bayern imeipisha Man United kileleni na kushika nafasi ya pili huku Arsenal na Liverpool zikiwa na idadi sawa ya wafuasi na kushika nafasi ya tatu.

Katika orodha ya jarida hilo, matajiri wa jijini Manchester, Manchester City, wamekamata nafasi ya tano.

Akizungumzia mafanikio hayo ya Man United kuipiku Bayern kwa umaarufu China, Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo, Jamie Reigle, alisema: “Likizo yetu China wakati wa majira ya kiangazi yaliweka mazingira mazuri katika kuungana na mashabiki na shughuli za kibiashara.

“Tulianzisha ushirikiano na vyombo vya habari China, tulitambulisha jezi zetu mpya tukiwa Shanghai na tulitambulisha bidhaa nyingi za wadhamini; hayo yalisaidia kuteka vyombo vya habari vya kidijitali.”

Katika hatua nyingine, ripoti ya Red Card iliitangaza Bundesliga kuwa ndiyo ligi inayofuatiliwa na mashabiki wengi wa soka nchini China.

Ligi Kuu England inashika nafasi ya pili, La Liga ni ya tatu, huku ile ya Ufaransa ya Ligue 1 ikikamata nafasi ya nne kwenye orodha hiyo ya timu zinazofuatiliwa na mashabiki wengi wa China kupitia mitandao.

Wayne Rooney ambaye amekuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na moja ya klabu kubwa za China, ameingia ‘top five’, sambamba na mchezaji mwenzake wa Man United, Anthony Martial.

Rooney ameshindwa kumpiku Ronaldo katika ripoti hiyo, licha ya taarifa za hivi karibuni kuwa wakala wake, Paul Stretford, ameshafika China kuangalia uwezekano wa nyota huyo kutua nchini humo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -