Saturday, November 28, 2020

KUMBUKA HAYA KABLA HUJAACHANA NAYE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Na Ramadhani Masenga,

JAPO wengi wanachukulia kawaida, ila suala la kuachana ni moja kati ya masuala nyeti sana. Hutakiwi kuchukua uamuzi huu haraka wala kwa shinikizo la mtu. Hili ni suala linalokuhusu wewe zaidi.

Kama likileta faida litaleta kwako na kama kukuathiri ni wewe utakayeathirika zaidi. Si suala la kuwaza na kuamua mara moja. Kama ilivyo muhimu sana kutulia kabla hujachukua uamuzi wa kuwa na fulani, hili pia ni jambo linalokuhitaji uwaze kwa kina kabla hujafikia uamuzi.

Nimeona wengi baada ya kuachana na wenza wao wakiwa katika hali tete kiakili na hata kimwonekano. Bila kuwaza sana, walikimbilia kuachana na matokeo yake wakiona wenzao wako na watu wengine huisi kama kuonewa au kudhalilishwa.

Huyo unayetaka kuachana naye baada ya kuondoka katika himaya yako anaweza kuwa katika himaya ya mtu mwigine. Umejiandaa vya kutosha kukubaliana na hilo? Kosa unaloamini linaenda kuwatenganisha, litafaa kukuweka katika kundi la faraja hata baada ya kuwa na mtu mwingine?

Acha kuwaza kinazi, waza kwa kina juu ya uamuzi wako. Ni kweli kuna baadhi suluhisho la furaha yao katika maisha ni kuachana tu. Je, na wewe unaamini kuwa kwa tabia ya mwenzako inafaa uachane naye?

Hapa si suala la kumng’ang’ania mtu hata kama unaona hakufai. Ila ni kweli hakufai kwa kiwango hicho? Kosa lake lina uzito wa kufanya utengano wenu uwe faraja katika maisha yako?

Mapenzi ni suala lako. Wewe na maisha yako. Linakuhusu wewe na furaha pamoja na huzuni yako. Hupaswi kuliamua haraka haraka. Jipe muda wa kutafakari masuala yako kwa kina.

Ni rahisi sana kuachana wakati mwingine, ila ni ngumu sana kuachana na mtu sahihi na kujihisi amani na utulivu. Kuna makosa mengine suluhisho si kuachana, kaa naye muyamalize.

Hata kama unahisi umekaa naye sana na bado haelekei kuwa unavyotaka, kabla hujaachana naye tafuta msaada kwa wataalamu au watu wenye busara katika kukuweka sawa kabla ya uamuzi wako.

Jua unapoachana naye anaenda kuwa na maisha mengine mbali na wewe. Hutakuwa na mamlaka naye kama ilivyo leo. Ndiyo, anakukera ila kuachana si suala jepesi kama kuweka chumvi nyingi katika mboga. Kuachana ni suala lililo kati ya furaha na huzuni yako. Fikiria kwa kina kama ukiachana naye utapata faraja au huzuni.

Si kila kosa kimbilio ni kuachana. Mengine ni kurekebishana na mambo kuwa kama unavyotaka yawe. Wengi mnaongozwa na jazba wakati mnachukua uamuzi. Baada ya kuona hali fulani haiko sawa, bila kufikiri mara mbili mnakimbilia katika kuachana. Ukiwa na hasira uamuzi huu utauona ni bora sana, ila zitaisha hizo na kuukabili ukweli. Hapo ndipo unaweza kujiona ulivyo juha.

Kuna watu mpaka leo wanalia kwa sababu ya kukimbilia kuachana. Waliachana na kuamini tofauti na matokeo yake wanaona tofauti. Kaa na mwenzako kabla hujaachana.

ungumzeni kwa kina kila kitu ambacho hakiko sawa baina yenu. Wengine labda jazba huwatawala hivyo mnashindwa kuzungumza kwa kina. Tafutateni msaada wa kitaalamu kabla hamjasema kila mtu na maisha yake. Kuachana ni rahisi sana ila amani baada ya kuachana huwa ngumu sana.

Ndiyo, kuna makosa halali yake ni kuachana, ila si kila kosa. Kuna kosa unaweza kuliona kuwa ni kubwa na kuamini ni bora mkaachana ila huenda unachangia pia katika kusababisha litokee. Suala si kukimbilia kuachana.

Jitahid kila unapoingia katika mtafaruku na mwenza wako kufikiria namna ya kutatua tatizo na si kukimbilia kuachana. Wengi wameachana kwa sababu wanapoona wenzao hawawaelewi wao hukimbilia katika kuachana. Hapo si sawa hata kidogo.

Kuna makosa ukiachana naye, hata kesho ukimkuta na mwingine bado utajipongeza kwa namna ulivyoamua ila si kila kosa. Mengine yamewafanya wakina fulani baada ya kuachana na kina nanihii, wakiwaona na wengine wanahisi kama wanasalitiwa.

Usipende kutamani kuachana, si suala zuri, halifurahishi na mara nyingi limeumiza wengi. Kila tatizo huwa na tiba yake. Itafuteni kwanza tiba ya mgogoro wenu kabla hujatamani kusema tuachane.

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -