Monday, November 30, 2020

KUNA HAJA KWA WASANII KUWA NA SEHEMU YA KUKUTANA NA KUPEANA TAARIFA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NI matumaini yangu kwamba mu-wazima wa afya. Tuko pamoja tena katika kulisukuma gurudumu la maendeleo ya sanaa za jukwaani hasa ya kudansi kupitia gazeti la BINGWA kwenye ukurasa huu.

Nawashukuru sana wadau ambao wamekuwa wakisoma na kuchangia maoni yao, au hata wale ambao wamekuwa wanasoma tu na kupata uelewa juu ya kile ninachokiandika. Lakini nasisitiza kuendelea kupata maoni yanu wasomaji juu ya maandiko haya na fani ya sanaa ya kudansi kwa ujumla.

Leo makala yangu nitayaelekeza kwenye eneo moja ambalo ni muhimu sana katika maendeleo ya fani yoyote ile. Sehemu ya kukutania wasanii ili kujadili kupanga mipango, kupeana taarifa na kuwezesha kazi za sanaa ziwe rahisi zaidi.

Hakuna kitu kizuri kama taarifa kwa dunia ya sasa na ili kuwepo na taarifa lazima kuwe na kituo ambacho wasanii wa aina fulani wanaweza kukutana ama iwe rasmi au isiwe rasmi ilimradi kuna sehemu maalumu wasanii wa aina fulani wanakutana na pia kuna taarifa zote za wasanii husika.

Kwa mfano Mango Garden, pale Kinondoni pangeendelezwa na kuboreshwa kwa makusudi, kwa maana wawepo watu maalumu wa kutunza na kuzitoa taarifa mbalimbali za wasanii kwa ukanda wa Kinondoni. Au Temeke pale TCC Club au kwa wasanii wa Temeke na Amana Vijana Centre au Max pale Bungoni kwa wasanii wa Ilala.

Kituo cha taarifa ni muhimu sana kwa wasanii wa ngazi zote, kujisajili pale Basata ni jambo moja, kufanya sanaa yako ukajulikana ni jambo la pili, lakini kupatikana au watu kupata taarifa zako hili ni jambo muhimu zaidi, maana hapo ndipo penye fursa mbalimbali.

Basata wanazo taarifa za wasanii waliowasajili, lakini kama wasanii inabidi kuwe na vituo maalumu ambavyo taarifa zao zitakuwapo, lakini pia wao watafika kupata taarifa mbalimbali na pia kuhusu taarifa zao ikiwa ni pamoja na kujadiliana juu ya masuala mbalimbali yanayowahusu na yanayohusu maendeleo yao.

Kukutana kwa wasanii kunaweza kubadilishana taarifa, msanii mmoja anaweza kumsaidia mwingine kupata taarifa fulani muhimu. Kuna ushauri kutoka kwa wanamuziki wakubwa kwenda kwa wadogo hili haliwezi kufanyika kwa simu pekee, kukiwa na sehemu ya kukutana itakuwa rahisi zaidi.

Sasa hivi watu wanafanya kazi na kupata taarifa kwa kutumia mitandao mbalimbali, sawa, lakini hizo taarifa zinatosha? Wapo watu maarufu hapa nchini kama vile wanamuziki, wacheza filamu, hawa unaweza kuzipata baadhi ya taarifa zao kwenye mitandao je, zinatosheleza?

Kama hazitoshelezi utazipata wapi habari zake kwa usahihi. Baadhi yao wana mameneja lakini hao mameneja wanapatikana? Ndio maana kuna haja ya kutengeneza klabu zitakazowakutanisha wasanii wa aina fulani.

Kupitia klabu hizi wasanii watabadilishana mawazo na kupeana elimu juu ya masuala mbalimbali na kuelezana miiko ya kazi. Lakini nani atawashauri kuhusiana na sauti kucheza watapata wapi dondoo za uzoefu na historia mbalimbali za kazi za sanaa kama hawakutani? Maisha ya sasa ni nadra sana watu kutembeleana, kama ni simu za mkononi si mara zote zinamaliza jambo.

Ni mihimu sana kwa wasanii kujenga utamaduni wa kukutana sehemu fulani inayochaguliwa na wahusika. Kukutana kwenu kunaweza kusababisha au likazalishwa jambo zuri sana na sanaa yetu ikasonga mbele mara dufu, haya yamefanyika sehemu mbalimbali duniani na kwa mafanikio makubwa, mfano mzuri ni Kenya pale Godown, ambapo pamekuwa sehemu kuu ya wasanii wa fani mbalimbali kukutana kuzungumza, kupeana taarifa na ushauri wa masuala mbalimbali. Tulitafakari hili na tuanze sasa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -